Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Real yamkata Enzo

Muktasari:

  • Baada ya Chelsea kushindwa kufuzu kushiriki michuano ya Ulaya msimu uliopita, vyanzo vinavyoaminika vimedai kuwa Fernandez anatamani kuondoka Stamford Bridge na kujiunga na Real Madrid.

MADRID,  Hispania: REAL Madrid imekanusha taarifa zinazoihusisha na mpango wa kumsajili kiungo wa Chelsea, Enzo Fernandez, katika dirisha hili la usajili.

Baada ya Chelsea kushindwa kufuzu kushiriki michuano ya Ulaya msimu uliopita, vyanzo vinavyoaminika vimedai kuwa Fernandez anatamani kuondoka Stamford Bridge na kujiunga na Real Madrid.

Miamba hiyo ya Hispania waliripotiwa kuvutiwa na kiungo huyo wa Argentina, ambaye Chelsea ilimsajili kutoka Benfica kwa ada ya pauni 107milioni mwezi Februari 2023, iliyokuwa rekodi ya uhamisho ghali zaidi nchini Uingereza wakati huo.

Hata hivyo, Real Madrid ilitoa taarifa rasmi Ijumaa ikisisitiza kuwa taarifa hizo “hazina ukweli wowote.”


Taarifa ya klabu hiyo ilisema:

“Kutokana na taarifa na kauli zilizochapishwa katika siku za hivi karibuni kuhusu madai ya Real Madrid kumtaka mchezaji Enzo Fernandez, klabu inapenda kuweka wazi kuwa haijafanya juhudi zozote, moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja, za kumsajili mchezaji huyo, na pia haina mpango wa kufanya operesheni hiyo.”

Kwa upande wake, Chelsea imethibitisha kuwa haijapokea mawasiliano yoyote rasmi kutoka Real Madrid kuhusu Fernandez.

Inadaiwa Chelsea inamthaminisha nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 kwa takriban pauni120 milioni iwapo kutakuwa na ofa ya kweli, lakini klabu hiyo haina mpango wa kumuuza na ingependelea aendelee kuwa mmoja wa wachezaji muhimu chini ya kocha mpya Xabi Alonso. Kocha wa zamani wa Chelsea, Liam Rosenior, alimpa Fernandez adhabu ya kutocheza mechi mbili mwezi Aprili baada ya mchezaji huyo kusema kuwa hana uhakika kama angebaki Chelsea msimu ujao na kuongeza kwamba “ningependa kuishi Madrid.”

Chelsea ilimsajili Fernandez kutoka Benfica muda mfupi baada ya kusaidia Argentina kutwaa Kombe la Dunia la tatu mwishoni mwa mwaka 2022.

Tangu hapo, amesaidia Chelsea kushinda Europa Conference Ligi na Kombe la Dunia la Klabu, huku akifunga mabao 15 katika mashindano yote msimu uliopita. Pia anaendelea kuwa mmoja wa wachezaji muhimu wa Argentina katika Kombe la Dunia la mwaka huu.

Majira haya ya joto, Real Madrid tayari imekamilisha usajili wa beki wa kushoto wa Hispania, Marc Cucurella kutoka Chelsea kwa mkataba wenye thamani ya hadi pauni51.8 milioni.