Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sababu zilizoziangusha timu saba za Afrika Kombe la Dunia

Muktasari:

  • Hata hivyo, wakati wakubwa wakiamua katika mechi za 16 bora, ni timu mbili pekee kutoka Afrika ambazo ni Misri na Morocco zilitoboa katika mashindano hayo kutinga hatua hiyo, baada ya saba zingine kuishia 32 bora na moja ilishindwa kutoboa kutoka kwenye kundi lake, Tunisia.

MIAMI, MAREKANI: HAKUNA kulala! Fainali za Kombe la Dunia 2026 zimeingia katika hatua ya 16 bora, ambapo tayari mechi mbili za kwanza zilipigwa usiku wa kuamkia leo, Canada imekiwasha dhidi ya Morocco, huku Paraguay na Ufaransa zikikabiliana kuamua inayofuzu kwa ajili ya robo fainali ya michuano hiyo.

Hata hivyo, wakati wakubwa wakiamua katika mechi za 16 bora, ni timu mbili pekee kutoka Afrika ambazo ni Misri na Morocco zilitoboa katika mashindano hayo kutinga hatua hiyo, baada ya saba zingine kuishia 32 bora na moja ilishindwa kutoboa kutoka kwenye kundi lake, Tunisia.

Timu za Afrika zimeshindwa kutomboa kwa wingi kama zilivyotinga 32 zikiwa nyingi kuliko mabara yote duniani (asilimia 96), kutokana na sababu kadhaa zilizoambatana na anguko hilo, kubwa ikitajwa kuwa ni mchanganyiko wa makosa ya kimkakati, uzoefu mdogo na kushindwa kutumia nafasi muhimu.

Ukiachana na Tunisia iliyoaga mapema katika hatua ya makundi, Afrika Kusini ndiyo iliyoanza kuaga 32 bora kwa kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Canada, ikifuatiwa na Ivory Coast iliyochapwa na Norway 2-1, Senegal ikararuriwa 2-3 na Ubelgiji, DR Congo ikafungwa 2-1 na England, Algeria 0-2 Uswisi, Cape Verde 2-3 Argentina na Ghana 0-1 Colombia.

Suala pelee muhimu linalojitokeza ni kwamba hakuna timu ya Afrika iliyofungwa kwa tofauti kubwa ya mabao na hii inaonyesha ushindani wa karibu, lakini pia ukosefu wa ‘wauaji katili’ katika vikosi vya timu hizo kama ilivyo kwa Argentina yenye Lionel Messi, England ina Harry Kane na Ufaransa ikiwa na Kylian Mbappe pamoja Ousmane Dembele ilhali Hispania ina Lamine Yamal.

Hiyo ina maana kwamba timu hizo zilikuwa zikikabiliana na ukosefu wa nyota walau mmoja kwenye vikosi wenye uwezo wa kuamua mechi katika nyakati ngumu na pia walinzi bora wenye mbinu za kisasa za kuhakikisha kwamba wanaweza kuishika mechi na kuzaidia upatikanaji wa ushindi.

Katika hilo, timu nyingi za Afrika zilikuwa na wachezaji wengi wanaocheza nje ya Afrika (ukiondoa Afrika Kusini) na miongoni mwao waliozaliwa Ulaya, lakini walishindwa kuzisaidia kuwa imara katika maeneo hayo.

Ni Ghana (yenye nyota wengi Ulaya) na Afrika Kusini (iliyokuwa ikianzisha mastaa watatu wanaocheza nje), ndizo zilizowapeleka puta wapinzani wao katika 16 bora na kuishia kufungwa bao 1-0 kila moja.

Hata hivyo, ilikuwa aibu zaidi kwa Senegal iliyozabwa mabao 3-2 iliyoongoza 2-0 kisha ikakubali Wabelgiji kurudisha na kupata ushindi ndani ya dakika 120 huku ikiwa na nyota wote uwanjani wanaocheza nje ya Afrika, suala ambalo liliibua hoja ya ufanisi katika kufanya uamuzi nyakati za mwisho mwisho za mchezo, kwani ilifungwa mabao karibu yote katika lalasalama.

Ukiachana na hayo kuna changamoto nyingine kubwa kwa timu za Afrika ilikuwa kushindwa kutumia nafasi zilizozitengeneza, na mfano ni Senegal iliyopata nafasi tatu za wazi kipindi cha pili, lakini ikafunga mara mbili tu, Ivory Coast ilitengeneza mashambulizi ya kasi lakini ilikosa umakini kwenye eneo la mwisho (final third), ilhali Ghana ilishindwa hata kupata bao licha ya kumiliki mpira kwa muda mrefu. Tatizo hilo linaonyesha pengo kati ya utengenezaji wa nafasi na kuzitumia ili kupata matokeo uwanjani.

Ipo pia hoja ya uzoefu wa hatua ya mtoano (knockout), ambapo timu zote saba zilionyesha udhaifu katika hilo zikicheza mechi zake kana kwamba zilikuwa zikishiriki hatua ya makundi, badala ya kuamini kwamba kosa moja linaweza kuzigharimu kwa kuondolewa mashindanoni.

Mtoano wa Kombe la Dunia ni tofauti kabisa na hatua ya makundi na ni hapa ambapo kila kosa huwa na gharama kubwa, mfano DR Congo ilionekana kukosa utulivu baada ya kufungwa bao la pili dhidi ya England, Afrika Kusini ilicheza vizuri lakini ilikosa ubunifu wa mwisho dhidi ya Canada huku Cape Verde ikikubali bao la mwisho dakika za mwisho dhidi ya Argentina. Makosa haya yote yalijitokeza baada ya dakika ya 70 na hivyo kwa Ivory Coast.