Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pogba adaiwa kusaini masika mbili Monaco

POGBA Pict

Muktasari:

  • Pogba, 32, alikuwa hana timu tangu alipokubali kusitisha mkataba wake na Juventus, Novemba mwaka jana baada ya kutumikia adhabu ya kufungiwa kucheza soka kwa kipindi cha miezi 18.

MONACO, UFARANSA: KIUNGO Paul Pogba anajiandaa kurejea kwenye soka, ikiripotiwa kukubali dili la miaka miwili kwenye klabu ya AS Monaco ya Ufaransa.

Pogba, 32, alikuwa hana timu tangu alipokubali kusitisha mkataba wake na Juventus, Novemba mwaka jana baada ya kutumikia adhabu ya kufungiwa kucheza soka kwa kipindi cha miezi 18.

Kiungo huyo wa zamani wa Manchester United, Pogba alikumbana na adhabu ya kufungiwa kucheza soka kwa miaka minne baada ya kupimwa na kukutwa ametupia virutubisho vya DHEA mwaka jana, lakini alishuhudia adhabu yake ikipunguzwa hadi miezi 18 na mahakama ya kimataifa ya rufani (CAS).

Pogba alikuwa na uwezekano wa kurudi uwanjani tangu Machi mwaka huu wakati adhabu yake ilipokwisha.

Sasa mshindi huyo wa Kombe la Dunia anaweza kurudi uwanjani baada ya kuposti picha yake akiwa mazoezini na kuandika: “Nadhani ni wakati”.

Kilichoelezwa staa huyo wa Ufaransa atasaini mkataba wa miaka miwili kwa ajili ya kuichezea Monaco msimu ujao. Monaco na Pogba waliafikiana tangu mwezi uliopita na msimu ujao anaweza kuonekana akiwa ndani ya jezi za miamba hiyo ya Ligue 1.

Hata hivyo, kuna baadhi ya mashabiki wanaamini Pogba anakwenda Bernabeu kujiunga na Real Madrid kwa kuwa staa huyo wa zamani wa Ligi Kuu England alionekana akiwa amevaa jezi ya miamba hiyo ya Hispania.

Shabiki mmoja aliandika: “Pogba anakwenda Real Madrid - Twende kazi”.

Mwingine aliongeza: “Karibu Real Madrid”.

Lakini, jambo hilo halipo hivyo kutokana na Pogba kuripotiwa ataonekana uwanjani msimu ujao akiwa Monaco. Mechi ya mwisho ya kimashindano Pogba kucheza ilikuwa Septemba 2023, alipotumika kwa dakika 28 katika mechi ya Juventus ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Empoli.