Pochettino atoa neno ushindi PSG

Monday January 11 2021
pochettino pic

MANCHESTER, ENGLAND. KOCHA Mauricio Pochettino amesisitiza kwamba kikosi chake kinapaswa kuongezeka ubora baada ya timu yake mpya ya Paris Saint-Germain kushinda 3-0 dhidi ya Brest juzi Jumamosi.

Watokea benchini Mauro Icardi na Pablo Sarabia waliongeza mabao juu ya lile alilotangulia kufunga Moise Kean wakati mabingwa watetezi hao wakipata ushindi wa kwanza chini ya kocha Pochettino.

Ushindi huo umekuja siku tatu tangu sare ya 1-1 dhidi ya Saint-Etienne katika mechi ya kwanza ya Pochettino madarakani, na kuipandisha PSG hadi pointi moja nyuma ya vinara Lyon, ambao walishikiliwa kwa sare ya 2-2 dhidi ya Rennes.

“Tumeridhishwa na ushindi, lakini kuna mengi ya kurekebisha,” alisema.

Advertisement