Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pesa ya Ronaldo katika Mitandao ya kijamii balaa

Muktasari:

  • Ronaldo pia ndiye mtu wa kwanza kufikisha wafuasi bilioni moja kwa mjumuisho katika kurasa zake za mitandao ya kijamii, na sasa anatamba na chaneli yake ya YouTube akiwa iitwayo UR Cristiano yenye wafuasi milioni 72.9.

RIYADH, SAUDI ARABIA: STAA wa AL Nassr, Cristiano Ronaldo ambaye ni mshindi mara tano wa tuzo ya Ballon d’Or, ni mmoja wa watu wenye nguvu katika upande wa mitandao ya kijamii hivi sasa akiwa ndio mtu mwenye wafuasi wengi zaidi katika upande wa  Instagram, akiwa na wafuasi milioni 647. 

Ronaldo pia ndiye mtu wa kwanza kufikisha wafuasi bilioni moja kwa mjumuisho katika kurasa zake za mitandao ya kijamii, na sasa anatamba na chaneli yake ya YouTube akiwa iitwayo UR Cristiano yenye wafuasi milioni 72.9.

Kwa nyakati tofauti, nyota huyo mwenye umri wa miaka 39 ameonekana kuweka machapisho ya matangazo ya taasisi na kampuni mbalimbali kama UFL, Saudi Arabia, AVA athletes, Whoop na Herbalife. 

Kwa sababu ya umaarufu wake na ukubwa wa akaunti yake hususani ya Instagram mikataba yake ya kutangaza kitu chochote huwa sio kinyonge.

Harry Hugo ambaye aliwahi kuwa mkuu wa mtandao wa Sportlobster ambao uliingia mkataba na Ronaldo kuwa balozi wao ametaja kiasi ambacho wakati huo walimlipa Ronaldo kuchapisha tangazo lao kwa mwaka mzima zaidi ya mara 30 hadi 40 ambacho kilikuwa ni kidogo sana ukilinganisha na mkwanja ambao kampuni sasa zinalipa ili kutangazwa na staa huyo.

“Tulikuwa watu wa kwanza kufanya mkataba wa kutangazwa mitandaoni na Cristiano Ronaldo, nakumbuka tulimlipa Pauni 250,000, hiyo ilikuwa ni kwa mwaka mzima, hapo alitakiwa kuchapisha karibu mara 30 hadi 40 ambapo pia ilikuwa inajumuisha kitufe cha kuelekeza watumiaji kwenda katika tovuti yetu,” alisema Hugo alipofanya mahojiano na Rising Ballers. 

“Kwa sasa inagharimu Pauni 1 milioni kwa kuchapisha tangazo lolote katika ukurasa wake wa Instagram jambo ambalo linatufanya tuamini tulipata bahati, ilifikia hatua kila wakati alipokuwa anachapisha tangazo tulipata karibia watu 2,000, wakati huo alikuwa na wafuasi milioni 100.” 

Kwa mujibu wa kitabu cha Football Leaks kilichoandikwa na waandishi wa Spiegel, Rafael Buschmann na Michael Wulzinger, Ronaldo na wakili wake walilipwa Pauni 920,000 na kampuni ya simu za Saudi, Mobily, kwa huduma ya saa nne na nusu ambapo kulikuwa na zoezi la upigaji picha, kusaini jezi tano pamoja na kuweka mambo hayo katika mitandao yake ya kijamii.

Taarifa kutoka CNN zinaeleza, mshambuliaji huyo anapata Pauni 2.57 milioni kwa kila chapisho moja  la Instagram ambayo analipwa na Instagram wenyewe.