Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nunez atoke, aje Alvarez Anfield

NUNEZ Pict

Muktasari:

  • Mabingwa wa Ligi Kuu England, Liverpool wamepania kufanya usajili mkubwa kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi na sasa wametakiwa kunasa saini ya mkali wa Atletico Madrid na mshindi wa Kombe la Dunia 2022, ambaye aliachwa na Manchester City mwaka mmoja uliopita.

LIVERPOOL, ENGLAND:STAA wa zamani wa Liverpool, Mjerumani Dietmar Hamann amesema italeta maana kama miamba hiyo ya Anfield itaachana na Darwin Nunez ili kumchukua staa wa Atletico Madrid, Julian Alvarez.

Mabingwa wa Ligi Kuu England, Liverpool wamepania kufanya usajili mkubwa kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi na sasa wametakiwa kunasa saini ya mkali wa Atletico Madrid na mshindi wa Kombe la Dunia 2022, ambaye aliachwa na Manchester City mwaka mmoja uliopita.

Alvarez amekuwa moto kwenye kikosi cha Atletico tangu alipotua kweye La Liga.

Alvarez alifunga mabao 29 katika kikosi hicho kinachonolewa na Diego Simeone, lakini amekuwa akihusishwa na mpango wa kurudi Ligi Kuu England. Na kwenye hilo, Hamann alisema dili la kubadilishana wachezaji ambalo litamhusisha Nunez, ambaye wamekuwa wa ziada tu huko Anfield, litakuwa na faida.

Nunez amekuwa akipambana na hali yake Liverpool. Anaendelea kuwa mchezaji ghali Liverpool kabla ya ujio wa Florian Wirtz, lakini mambo yake ya uwanjani yamekuwa na majanga makubwa kwa kipindi cha misimu mitatu aliyokuwa na miamba hiyo.

Hamann alisema: “Ningependa kumuona Julian Alvarez kwenye kikosi cha Liverpool na nadhani Darwin Nunez anaweza kuwa sehemu ya dili hilo na italeta maana. Nadhani Nunez ametengenezwa kwa ajili ya Atletico Madrid kutokana na soka lake la kutumia nguvu, anayependa mapambano akiwa ni aina ya wale ambao Diego Simeone anawataka.

“Alvarez anaweza kuwa kitu kizuri Liverpool, alikuwa kwenye kivuli cha Erling Haaland pale Manchester City, lakini tayari amejitengenezea hadhi yake Madrid. Anaongoza safu ya ushambuliaji, anafunga mabao, nadhani utakuwa usajili mzuri.

“Kumekuwa na uvumi wa kuhusu washambuliaji wengine, lakini Alvarez utakuwa usajili mzuri Liverpool na Nunez anaweza kuwa usajili bora Atletico.”

Alvarez alitamba kwenye Ligi Kuu England, ambapo kwa miaka miwili aliyotumikia Man City alifunga mabao 36, lakini alikuwa chaguo la pili kwenye fowadi ya kocha Pep Guardiola mbele ya Erling Haaland.