Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Panga la Guardiola kumfyeka Grealish Man City

Panga Pict

Muktasari:

  • Kocha Pep Guardiola amepanga kupitisha panga kwa wachezaji ambao viwango vyao vimeshuka huku hilo likitarajiwa kufanyika kwenye dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi.

MANCHESTER, ENGLAND: STAA ghali kabisa kwenye Ligi Kuu England, Jack Grealish ametajwa ndiye mchezaji atakayeongoza kundi la mastaa wasiopungua wanane watakaofunguliwa mlango wa kutokea huko Manchester City.

Kocha Pep Guardiola amepanga kupitisha panga kwa wachezaji ambao viwango vyao vimeshuka huku hilo likitarajiwa kufanyika kwenye dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi.

Man City ilitupwa nje ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na Real Madrid, Jumatano iliyopita.

Kufeli kwao kwenye michuano ya Ulaya kulitanguliwa na timu hiyo kutupwa nje kwenye Kombe la Ligi huku pia mambo yakiwa magumu kwenye kutetea ubingwa wao wa Ligi Kuu England.

Matumaini pekee ya kikosi hicho kubeba taji msimu huu yapo kwenye Kombe la FA na kwenye raundi ya tano watamenyana na timu ya daraja la chini, Plymouth Argyle, Machi 1.

PAN 01

Man City ilitumia pesa kwenye usajili wa Januari wakati ilipowanasa Omar Marmoush, Nico Gonzalez, Abdukodir Khusanov na Vitor Reis. Lakini, kusajili dirisha lijalo, timu hiyo itahitaji kupiga chini mastaa wake.

Kinachoelezwa, kuna wachezaji wanane watafunguliwa mlango wa kutokea ili wapya waje.

Kwenye orodha hiyo, watakuwamo Grealish, Kevin De Bruyne, Bernardo Silva, John Stones, Mateo Kovacic, Ilkay Gundogan na Ederson.

Kyle Walker anatarajia kuondoka jumla baada ya sasa kucheza kwa mkopo huko AC Milan. Wachezaji wote hao umri wao unaanzia miaka 30 kwenda juu, kitu ambacho kinamsukuma Guardiola awafungulie mlango wa kutokea kwa lengo la kuleta vijana zaidi kwenye kikosi chake.

Msimu huu ni kama vile umeshakwisha kwao na sasa Guardiola anafikiria mambo ya msimu ujao. Kwa sasa imani yake ipo kwa mastaa wanne aliowasajili kwenye dirisha la Januari, akiamini na wengine watakaokuja mwisho wa msimu watarudisha makali ya kikosi hicho cha Etihad.

PAN 02
PAN 02

Kwenye dirisha lijalo la majira ya kiangazi, Man City itampokea kikosini Juma Bah iliyomsajili Real Valladolid na kumtoa kwa mkopo RC Lens hadi mwisho wa msimu. Na kikosi hicho kwa sasa kipo kwenye mbio za kufukuzia saini ya mchezaji wa Pauni 85 milioni, Florian Wirtz kutoka Bayer Leverkusen, ambaye wanamtazama kama 'De Bruyne mpya'. Kikosi cha sasa na Man City kina wastani wa umri wa miaka 26.6.

HUU HAPA UMRI WA MASTAA WA MAN CITY

Makipa:

Ederson, 31

Stefan Ortega, 32

Scott Carson, 39


Mabeki:

Ruben Dias, 27

Manuel Akanji, 29

Nathan Ake, 30

John Stones, 30

Vitor Ries, 19

Abdukodri Khsanov, 20

Jahmai Simpson-Pursey, 19

Josko Gvardiol, 23

Rico Lewis, 20

Kyle Walker, 34


Viungo:

Rodri, 28

Mateo Kovacic, 30

Nico Gonzalez, 23

Ilkay Gundogan, 34

Bernardo Silva, 30

Kevin de Bruyne, 33

Claudio Echeverri, 19

James McAtee, 22


Washambuliaji:

Jeremy Doku, 22

Jack Grealish, 29

Phil Foden, 24

Savinho, 20

Oscar Bobb, 21

Erling Haaland, 24

Omar Marmoush, 26

Wastani wa umri: 26.6