Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Palmer ni rekodi tu huko Chelsea

Muktasari:

  • Kiungo huyo mshambuliaji mwenye umri wa miaka 22 alicheza mechi yake ya 60 kwenye kikosi cha The Blues na kufunga bao, akiasisti na kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa mechi wakati Chelsea ilipopata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Aston Villa.

LONDON,ENGLAND: STAA, Cole Palmer bado hajabeba mataji kulingana na magwiji wa zama za karibuni kwenye kikosi cha Chelsea, lakini Mwingereza huyo amekuwa mchezaji muhimu kwa rekodi za kibabe kabisa huko Stamford Bridge.

Kiungo huyo mshambuliaji mwenye umri wa miaka 22 alicheza mechi yake ya 60 kwenye kikosi cha The Blues na kufunga bao, akiasisti na kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa mechi wakati Chelsea ilipopata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Aston Villa.

Bao alilofunga Palmer kwenye mchezo huo lilikuwa la 33 na asisti aliyotoa ilikuwa ya 21 tangu alipotua kujiunga na timu hiyo kwa ada ya Pauni 40 milioni akitokea Manchester City mwanzoni mwa msimu uliopita.

Mwaka wake wa kwanza huko West London, staa huyo wa Englanbd alifunga mabao 22 na kushika namba mbili nyuma ya Erling Haaland kwenye mbio za kuwania Kiatu cha Dhahabu cha Ligi Kuu England msimu uliopita.

Ameendelea na kiwango bora kabisa msimu huu, akifunga mabao manane katika mechi 13. Kiungo huyo mshambuliaji amekuwa na uwezo mkubwa wa kufunga na kushindana na mastraika. Bao lake alilofunga dhidi ya Aston Villa lilikuwa na 30 kwenye Ligi Kuu England akiwa na Chelsea.

Amefanya hivyo kwenye mechi 46 tu, huku akiwa amezidiwa na Jimmy Floyd Hasselbaink pekee aliyefikisha idadi kama hiyo ya mabao akiwa amecheza mechi chache, 41. Lakini, Palmer kwenye mabao yake 30 amemzidi Diego Costa kwa mechi mbili na Didier Drogba kwa mechi 21.

Magwiji wengine hao wote waliisaidia Chelsea kubeba ubingwa kwenye misimu yao ya kwanza, hivyo Palmer ana kibarua kufikia anga hizo.

Linapokuja suala la kufunga na kuasisti ndani ya mwaka mmoja, staa huyo anayevaa jezi Namba 20 anahitaji matatu zaidi kuweka rekodi klabuni.

Palmer amehusika kwenye mabao 34 huku kukiwa bado na mechi sita zimebaki kwenye Ligi Kuu England kumaliza mwaka 2024.

Hasselbaink, ambaye alifanya hivyo mwaka 2001, alihitimisha mwaka huo kwa rekodi ya mabao 36.

Tangu Palmer alipocheza mechi yake ya kwanza Chelsea, ambayo ilichapwa 1-0 na Nottingham Forest, Septemba 2023, amehusika kwenye mabao 47, ikiwa ni mengi kuzidi mchezaji mwingine yeyote kwenye kikosi cha Chelsea ndani ya muda huo.