Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Owen Hargreaves: Viungo watatu ni dawa Man United

OWEN Pict

Muktasari:

  • Mashetani Wekundu walipata ushindi wa nne mfululizo chini ya nyota wao wa zamani dhidi ya Spurs waliopungukiwa na mchezaji mmoja katika mechi hiyo iliyofanyika Old Trafford na wenyeji kushinda mabao 2-0.

MANCHESTER, ENGLAND: OWEN Hargreaves amesema Michael Carrick hatimaye ametatua tatizo la kiungo la Manchester United, akimsifu Bruno Fernandes kwa kiwango cha ajabu alichokiita ni cha kushtua kabisa.

Mashetani Wekundu walipata ushindi wa nne mfululizo chini ya nyota wao wa zamani dhidi ya Spurs waliopungukiwa na mchezaji mmoja katika mechi hiyo iliyofanyika Old Trafford na wenyeji kushinda mabao 2-0.

Bryan Mbeumo aliipa Man United mwanzo mzuri baada ya nahodha wa Tottenham, Cristian Romero, kutolewa nje kwa kadi nyekundu kufuatia faulo mbaya dhidi ya Casemiro. Bruno Fernandes kisha aliongeza bao la pili na kufikisha mchango wake wa mabao na asisti 200 tangu ajiunge na klabu hiyo.

Staa wa zamani wa Man United, Hargreaves, sasa anadai kuwa safu ya kiungo ya klabu hiyo imekuwa nguvu yao kubwa, baada ya kuwa dhaifu chini ya kocha wa zamani Ruben Amorim. Pia alitoa sifa za kipekee kwa kiungo huyo wa Kireno kufuatia kiwango chake bora cha hivi karibuni.

Akizungumza na TNT Sports, amesema: “Tuwe wa kweli, mchango wa mabao 200 ni kitu cha kushangaza sana. Hizo ni takwimu za PlayStation. Anacheza kwa hatari, lakini ni hatari ambayo timu inanufaika nayo.

“Kobbie (Mainoo) nyuma yao alikuwa mzuri tena, na Casemiro… hao watatu pengine ndio walikuwa wachezaji bora zaidi katika mchezo huu, kwa maoni yangu. Tulikuwa tukisema hapo awali, chini ya Ruben Amorim, safu ya kiungo ilikuwa dhaifu, lakini hawa viungo watatu ni wazuri sana. Ni wazi Bruno ndiye mchezaji bora kwa mbali sana na nadhani sasa wanaonekana imara zaidi kama safu ya viungo watatu.”

Hata hivyo, Fernandes hataki wachezaji wenzake wapumzike kwenye mafanikio yao na amesisitiza kuwa sasa wanapigania ushindi wa tano mfululizo.