Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ndoto ya Michel Nkuka  ‘Lumumba’ yazimika njiani

LUMUMBA Pict

Muktasari:

  • Ndio, michuano hiyo ya 35 tangu ilipoasisiwa mwaka 1957, haihusiani tu na mabao na vikombe, bali inahusiana na hadithi, uso na hisia zinazotoa roho ya kipekee kwa mashindano.

RABAT MOROCCO: MICHUANO ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 imefikia patamu baada ya kumalizika kwa mechi za 16 Bora na sasa ngoma imeingia robo fainali, lakini ndoto za Wakongomani hususani shabiki Michel Nkuka Mboladinga anayemuenzi Patrice Lumumba, zimeisha njiani baada ya Algeria kuwang'oa michuanoni 'jionii'.

Ndio, michuano hiyo ya 35 tangu ilipoasisiwa mwaka 1957, haihusiani tu na mabao na vikombe, bali inahusiana na hadithi, uso na hisia zinazotoa roho ya kipekee kwa mashindano.

Wengine waliouakisi zaidi roho hiyo ni shabiki mashuhuri wa DR Congo, Lumumba ambaye uwepo wake wa shauku ulipendeza vema katika viwanja vya michezo yote ya mashindano.

Usiku wa juzi ambao safari ya DR Congo ilipofika tamati kwa moyo kuvunjika kutokana na Algeria, Lumumba alikuwa mfano wa ibada safi na hatimaye, huzuni kubwa.

Anajulikana kwa kusimama wakati wote wa mchezo, kuongoza nyimbo na kuhamasisha mashabiki wa DR Congo, tena alikataa kukaa, akiihimiza timu yake kutoka filimbi ya kwanza hadi ya mwisho.

Lakini soka linaweza kuwa gumu. Wakati Algeria ilipofunga bao la dakika za mwisho katika muda wa ziada wa mechi hiyo iliyichezwa kwa dakika 120, uwanja uliripuka na hisia pia.

Lumumba alitumbukia katika machozi, bila faraja, ndoto ikipotea kwa njia ya maumivu makali. Wazuri waliomzunguka walijaribu kumfariji mtu ambaye alitumia mashindano yote kuinua morali ya mashabiki.

Athari yake haikuonekana kuwa ndogo. Kabla ya kuanza kwa mchezo, Rais wa CAF, Patrice Motsepe, alimshukuru binafsi Lumumba, akimsifu kwa kuleta rangi, shauku na furaha katika viwanja na kufanya uzoefu wa kutazama DR Congo kuwa wa kipekee zaidi kwa mashabiki kote Afrika.

Wakati kampeni ya DR Congo imekwisha, picha ya Lumumba akiwa amesimama itabaki kuwa mojawapo ya kumbukumbu za kudumu za AFCON hii. Katika ushindi na kwenye kupoteza, aliwakumbusha kila mtu kwamba soka ni kuhusu watu walioko kwenye viti vya mashabiki kadri inavyohusu wachezaji uwanjani.

Bao lililozima ndoto za Lumumba, liliwekwa kimiani dakika ya 119 na mtokea benchi Adil Boulbina akimalizia pasi muru ya Ramiz Zerrouki, ikiwa ni dakika sita tu tangu mfunmgaji huyo aingie uwanjani akimpokea Fares Chaibi dakika ya 113 na kuing'oa DR Congo na kuifuata Nigeria katika mechi ya robo fainali wikiendi hii.