Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Shabiki anayemwigiza Lumumba ashangaza AFCON

SHABIKI Pict

Muktasari:

  • Congo ilifuzu kwenda hatua ya 16 bora ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) Jumanne usiku baada ya kuifunga Botswana mabao 3-0 na tangu hapo  sherehe za mashabiki wa DRC uwanjani na nyumbani zimeenea kwa kasi mitandaoni.

RABAT, MOROCCO: SHABIKI mmoja wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) amesambaa kwa kasi mitandaoni kutokana na heshima ya kipekee aliyotoa katikati ya mchezo kwa Waziri Mkuu wa kwanza wa nchi hiyo, Patrice Lumumba  Lumumba aliuawa mwaka 1961.

Congo ilifuzu kwenda hatua ya 16 bora ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) Jumanne usiku baada ya kuifunga Botswana mabao 3-0 na tangu hapo  sherehe za mashabiki wa DRC uwanjani na nyumbani zimeenea kwa kasi mitandaoni.

Hata hivyo, kilichovutia wengi ni heshima aliyotoa shabiki mmoja mahiri wa timu hiyo kwa marehemu Lumumba ndiyo imevutia zaidi hisia za watu kwenye mitandao ya kijamii.

Kuka Mboladinga alijizolea umaarufu mitandaoni baada ya kusimama kwa muda wote wa mechi akiwa katika mkao uleule wa sanamu maarufu ya Lumumba, iliyopo Kinshasa.

Mboladinga, anayefanana kwa kiasi kikubwa na Lumumba, alivaa koti na tai kama ishara ya heshima kwa Waziri Mkuu wa kwanza wa nchi hiyo aliyeingia madarakati baada ya kupata uhuru kutoka Ubelgiji mwaka 1960.

Shabiki huyo alisimama huku mkono wake wa kulia ukiwa juu kwa dakika 115 mfululizo kabla ya kushuka kutoka kwenye jukwaa alilojitengenezea.

SHABI 02

Kitendo hicho cha ajabu cha uvumilivu kiliwashangaza mashabiki wa soka waliokuwa wakitazama mechi hiyo kote duniani.

Mmoja aliandika kwenye mtandao wa X: “Huu ni uzalendo wa hali ya juu kabisa.”

Mwingine amesema: “DRC inahitaji kufuzu Kombe la Dunia ili tumpeleke Lumumba ng’ambo ya bahari!”

Mwingine akaongeza: “Hili ni jambo zuri sana. Viongozi kama  Patrice Lumumba wanapaswa kuenziwa milele.  Na tunapaswa kuwafundisha watoto wetu kuhusu wao."

 Mboladinga alifanya hivyo pia katika mechi ya kwanza ya Congo kwa hatua ya makundi dhidi ya Benin, mechi yapili mbele ya Senegal na mwisho mbele ya Botswana.

Inaelezwa kuwa huenda akawa miongoni mwa mashabiki wa DRC watakaohudhuria mechi ya hatua ya 16 bora dhidi ya Algeria, ambapo kikosi cha Sebastien Desabre kitacheza Jumanne ya wiki  ijayo.