Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nadal njia panda Olimpiki 2023

Muktasari:

  • Nadal aliyesumbuliwa na majeraha ya muda mrefu, aliporomoka hadi nafasi ya 275 kwenye ubora wa tenisi kiasi cha kukosa kigezo cha kushiriki michuano hiyo mbele ya nyota wenzake wa Hispania, Carlos Alcaraz, Alejandro Fokina na Pedro Martinez aliyeponda nafasi yake kutwaliwa na Nadal.

LICHA ya kuporomoka kwenye viwango vya ubora wa tenisi ya wanaume duniani, nyota Rafael Nadal ametumia nafasi ya kipekee ili kushiriki michuano mikubwa ijayo ya Olimpiki ya Paris, Ufaransa.

Nadal aliyesumbuliwa na majeraha ya muda mrefu, aliporomoka hadi nafasi ya 275 kwenye ubora wa tenisi kiasi cha kukosa kigezo cha kushiriki michuano hiyo mbele ya nyota wenzake wa Hispania, Carlos Alcaraz, Alejandro Fokina na Pedro Martinez aliyeponda nafasi yake kutwaliwa na Nadal.

Bingwa huyo mara 22 wa mataji makubwa (Grand slam) duniani, anataka kushiriki michuano hiyo ya olimpiki na bila shaka itakuwa ya mwisho kwake kutokana na kuwa mbioni kustaafu mchezo huo.

Nadal ametoka kutolewa na Alexander Zverev kwenye raundi ya kwanza michuano ya wazi Ufaransa.