Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nadal kufuata nyayo za Federer

Muktasari:

  • Majeraha ya hapa na pale yaliyokua yanampata yalimlazimu staa huyo kutangaza kuachana na tenisi akiwa na mataji makubwa (Grand slam) 20 nyuma ya wakali wenzake Rafael Nadal na Novak Djokovic ambao wana 22 na 24 mtawalia.

MWAKA 2022 aliyekuwa nyota wa mchezo wa tenisi duniani, Roger Federer kutoka Uswizi ndiye alitangaza kustaafu mchezo wa tenisi.

Majeraha ya hapa na pale yaliyokua yanampata yalimlazimu staa huyo kutangaza kuachana na tenisi akiwa na mataji makubwa (Grand slam) 20 nyuma ya wakali wenzake Rafael Nadal na Novak Djokovic ambao wana 22 na 24 mtawalia.

Federer alitumia michuano ya Laver cup ya Uingereza kipindi kama hiki kutangaza kustaafu tenisi na utamu zaidi ni kucheza mchezo wa kuaga sanjari na Nadal katika mchezo wa double na sasa dalili nyingine zinaanza kutokea kwa Nadal ambaye bado hatma ya kustaafu kwake haijafahamika ataitangazia wapi.

Tayari Nadal ameorodheshwa kushiriki michuano hiyo ya Septemba, akiwa ametoka kuipiga chini michuano mikubwa ya Wazi ya Marekani (US OPEN).