Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwanetu Joao Felix amepoa hapa!

FELIX Pict

Muktasari:

  • Fowadi huyo wa kimataifa wa Ureno alijiunga na Chelsea wakati wa dirisha la majira ya kiangazi la mwaka jana akitokea Atletico Madrid kwa ada ya uhamisho ya Pauni 42 milioni.

MIAMI, MAREKANI: STAA wa Chelsea, Joao Felix hatimaye ameanza kutupia nyavuni baada ya kufanikiwa kumnasa mrembo matata kabisa wa Colombia, Valentina Rueda Velez.

Fowadi huyo wa kimataifa wa Ureno alijiunga na Chelsea wakati wa dirisha la majira ya kiangazi la mwaka jana akitokea Atletico Madrid kwa ada ya uhamisho ya Pauni 42 milioni.

Felix, 25, alisaini mkataba huko Stamford Bridge utakaokomea 2031, lakini aliishia kufunga mara moja tu kwenye Ligi Kuu England, katika mechi yake ya kwanza dhidi ya Wolves - kabla ya kutolewa kwa mkopo kwenda AC Milan kwenye dirisha la Januari.

Mambo yalivyokuwa magumu ndani ya uwanja na hata nje ya uwanja ilikuwa hivyo pia, ambapo staa huyo aliripotiwa kuwa singo tangu alipoachana na mrembo mwingizaji Margarida Corceiro mwaka 2023.

Lakini, hivi karibuni alipigwa picha akiwa na mkali wa runinga, mrembo Valentina Rueda Velez wakati alipokwenda mapumziko huko Miami mapema mwezi huu.

Mrembo Valentina, ambaye pia ni mwanamitindo aliwahi kuonekana kwenye shoo ya mambo ya uhusiano ya Netflix inayofahamika kwa jina la Too Hot To Handle.

Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 24 aliposti video mtandaoni aliyokuwa na mwanasoka huyo huko Florida kabla ya kuishusha video hiyo. Huo ni ushindi wa Felix nje ya uwanja unaompa nafasi ya kutulia kwa Valentina.

Mambo ya uwanjani hayakuwa mazuri huko San Siro na hivyo kujikuta akienguliwa kwenye kikosi cha Chelsea kilichokwenda Marekani kwenye fainali za Kombe la Dunia la Klabu, huku jezi yake Namba 14 aliyokuwa akivaa, nayo imekabidhiwa kwa mchezaji mpya, Dario Essugo.

Staa Felix amei-chezea timu ya taifa ya Ureno mechi 45 na kufunga mara tisa.