Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtalii Balotelli ajiunga klabu ya 14 kwenye soka

BALOTELLI Pict

Muktasari:

  • Fowadi huyo Mtaliano aliyetumikia nusu ya kwanza ya msimu huu akiwa mchezaji huru baada ya kuondoka Genoa mkataba ulipofika tamati Juni mwaka jana.

ROME, ITALIA: SUPASTAA straika Mario Balotelli sasa amekamilisha mpango wake wa kujiunga na klabu ya 14 katika maisha yake ya soka baada ya kuibukia Al-Ittifaq ya Dubai.

Fowadi huyo Mtaliano aliyetumikia nusu ya kwanza ya msimu huu akiwa mchezaji huru baada ya kuondoka Genoa mkataba ulipofika tamati Juni mwaka jana.

Balotelli amezivutua timu nyingi za Major League Soccer na Liga MX dirisha lililopita la majira ya kiangazi, lakini alishindwa kupata ya kujiunga nayo.

Staa huyo, 35, alitunza kiwango alipokuwa akicheza na kuwa kocha huko Kandima, Maldives, na sasa amepata timu ya kuitumikia.

Balotelli amesaini mkataba wa miaka miwili na nusu Al-Ittifaq. Hii sio ile timu ya Saudia aliyoinoa Steven Gerrard. Ni ya Falme za Kiarabu, ilianzishwa miaka sita iliyopita na sasa inashika mkia kwenye ligi ya UAE First Division.

Al-Ittifaq imeshinda mechi mbili kati ya 11 msimu huu, huku ikiwa imefunga mabao sita. Hata hivyo, straika huyo ambaye zama zake Ulaya zinaonekana kumpa kisogo, alishindwa kufunga bao lolote katika mechi sita Genoa  msimu uliopita.

Na sasa timu hiyo inakuwa ya 14 tangu uhamisho wa kujiunga na Inter Milan 2007 wakati huo alipokuwa kinda akitokea Lumezzane.

Alikuwa sehemu ya kikosi kilichoshinda mataji matatu makubwa msimu mmoja chini ya kocha Jose Mourinho.  Asisti yake maarufu Ligi Kuu England ni ile ya bao la Sergio Aguero, ambalo liliifanya Manchester City kunyakua taji hilo 2012.

Baada ya kutibuana na kocha wa Man City, Roberto Mancini, Balotelli alikwenda AC Milan. Baadaye, alirudi Ligi Kuu England akijiunga na Liverpool 2014.

Kisha alijiunga na Nice ya Ufaransa baada ya mkopo AC Milan. Tangu wakati huo hajadumu timu moja zaidi ya msimu mmoja akipita Ligue 1, Serie A, Uswisi na Uturuki.