Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Duh! Sikia hii ya Balotelli

BALOTELI Pict

Muktasari:

  • Fowadi huyo wa zamani wa Manchester City na Liverpool aliwahi kuwa mshindi wa taji la Ligi Kuu England na aliwahi kuichezea timu ya taifa ya Italia mechi 36.

MADRID, HISPANIA: MAISHA yanakwenda kasi sana. Ndiyo hivyo, straika Mario Balotelli yupo kwenye hatua za mwisho za kujiunga na timu ya Daraja la Tatu huko Hispania.

Fowadi huyo wa zamani wa Manchester City na Liverpool aliwahi kuwa mshindi wa taji la Ligi Kuu England na aliwahi kuichezea timu ya taifa ya Italia mechi 36.

Lakini, Balotelli maisha yake yalibadilika tangu alipoondoka Anfield muongo mmoja uliopita, huku akiwahi kucheza soka kwenye nchi za Uturuki na Uswisi.

Staa huyo mwenye umri wa miaka 34 alijiunga na Genoa ya Italia, Oktoba mwaka jana, lakini aliachwa na timu hiyo baada ya kucheza mechi sita tu. Wakala wake kwa sasa ameanzisha mazungumzo na Real Murcia, ambayo ipo kwenye Ligi Daraja la Tatu huko Hispania.

Rais wa Murcia, Felipe Moreno alikutana na mawakala wa Balotelli huku Madrid kujadili dili hilo wakiwa sambamba na mkurugenzi wa michezo wa klabu, Asier Goiria.

Moreno ameripotiwa kuwa tayari kumchukua Balotelli, ambaye atatimiza miaka 35 mwezi ujao.

Murcia iliwahi kucheza La Liga kwa misimu 18 huku mara yao ya mwisho ilikuwa msimu wa 2007-08, huku ikiwa na rekodi ya kushinda ubingwa ya Segunda mara nane.

Tatizo la uchumi liliwafanya kushuka hadi kufikia Daraja la Nne mwaka 2022.

Ilipambana na kurudi Daraja la Tatu na mambo yangekuwa tofauti kama wasingepoteza kwenye mechi ya mchujo msimu uliopita. Inatumia uwanja wenye uwezo wa kuingiza watazamaji 31,000, Estadio Nueva Condomina, huku wadai wakiamini msimu ujao inaweza kupanda daraja.

Mambo mengi ya nje ya uwanja yamedaiwa kutibua maisha ya soka ya Balotelli.