Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Merino atuma ujumbe huko, asisitiza jambo

MERINO Pict

Muktasari:

  • Arsenal itakuwa timu ya kwanza katika ligi ya juu kucheza mechi nne mfululizo za ugenini katika mashindano manne tofauti ndani ya kipindi cha siku kumi.

LONDON, ENGLAND: KIUNGO mwenye uwezo mkubwa wa kufunga, Mikel Merino amesema kwa msisitizo Arsenal iko tayari kupambana na msongamano wa ratiba yao ya mechi kwa sababu wana ‘njaa’ ya kushinda mataji msimu huu.

Arsenal itakuwa timu ya kwanza katika ligi ya juu kucheza mechi nne mfululizo za ugenini katika mashindano manne tofauti ndani ya kipindi cha siku kumi.

Waliishinda Portsmouth katika Kombe la FA, Jumapili, watakutana na Chelsea katika mechi ya kwanza ya nusu fainali ya Kombe la Ligi, Jumatano, kisha watasafiri kwenda Nottingham Forest, Jumamosi katika mbio za ubingwa wa ligi, kabla ya kukabiliana na Inter Milan katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, Jumanne ijayo.

MERI 01

Ni ratiba inayochosha sana ambayo itapima uimara na azma ya kikosi cha Mikel Arteta, lakini Merino anasema wachezaji wote wamedhamiria kushinda mataji msimu huu.

Kocha Arteta, ana kombe moja tu la FA tangu alipoteuliwa mwaka 2019, lakini msimu huu Arsenal ipo katika mchanganyiko wa kushinda mataji manne.

MERI 02

Ndiyo maana Merino anasema Arsenal watachukulia kila mechi kwa uzito na kulenga ushindi bila kujali mashindano wanayoshiriki.

Kiungo huyo Mhispaniola, Merino, amesema: “Njaa ipo. Imekuwepo kwa muda mrefu. Wakati mwingine ni suala la mambo madogo, hali fulani, dakika fulani, au nyakati fulani ambazo hukuzuia kushinda. Lakini njaa hiyo ipo, na unaweza kuiona katika kila mazoezi. Nayo itakuwepo hadi mwisho wa msimu.”

MERI 03

Merino pia alieleza kurejea kwa Kai Havertz, aliyekuwa majeraha, kama nyongeza ya ajabu kwenye kikosi, huku akisema kina cha kikosi kinawapa matumaini ya kuendelea kupigania ushindi katika mashindano yote manne licha ya ratiba ngumu.

Merino aliongeza: “Ni jambo la ajabu kabisa. Sote tumefurahia sana kurejea kwa Kai baada ya jeraha kubwa sana. Kuwepo kwake ni faida kubwa kwa kila mtu kwa hali ya hewa kambini, kwa mchango anaoutoa mazoezini, na uwepo wake katika kila kikao cha mazoezi. Sasa kumwona uwanjani ni nyenzo nyingine muhimu, chaguo jingine kwa kocha. Tunafurahia sana kwa ajili yake.”