Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal kila kitu kipo vizuri 2026

ARSENAL Pict

Muktasari:

  • Kikosi hicho cha kocha Mikel Arteta kimeanza Mwaka Mpya 2026 kikiongoza msimamo wa Ligi Kuu England kwa tofauti ya pointi nne. Na sasa, Arsenal inapewa nafasi kubwa ya kubeba taji hilo, kumaliza ukame wa miaka 23.

LONDON, ENGLAND: ARSENAL imefunga mwaka 2025 kibeba sana huku ikiamini 2026 itakuwa bora zaidi kwao.

Kikosi hicho cha kocha Mikel Arteta kimeanza Mwaka Mpya 2026 kikiongoza msimamo wa Ligi Kuu England kwa tofauti ya pointi nne. Na sasa, Arsenal inapewa nafasi kubwa ya kubeba taji hilo, kumaliza ukame wa miaka 23.

Hata hivyo, kuna baadhi ya wachezaji wao wamekuwa na mchango mkubwa sana kwa kile kilichotokea kwenye kikosi hicho na kocha Arteta anaomba waendelee kumwaga moto.

Lakini, je ni wachezaji hao kama ni alama, wamepata ngapi kwa kuzingatia mchango wa 2025.

-David Raya – 8/10; Akilindwa na safu imara ya mabeki, kipa Raya amefanya mambo makubwa sana, akifanya sevu muhimu zinazoifanya Arsenal iendelee kukaa kileleni hadi sasa.

-Kepa – 6/10; Amecheza mechi tatu tu, zote kwenye Kombe la Ligi, hivyo ni ngumu kumjadili sana juu ya mchango wake kwenye Ligi Kuu England.

EP 02

-Ben White – 6/10; Majeraha yanamtibulia mengi. Lakini, mara zote anapokuwa uwanjani, amekuwa akitoa mchango mkubwa hasa kwenye beki ya kulia.

-Cristhian Mosquera – 7/10; Aliwasaili wakati wa dirisha la kiangazi na hakika amekuwa mchezaji muhimu kwenye beki ya Arsenal, akiongeza utulivu mkubwa katika safu hiyo.

-Gabriel – 8/10; Kama asingepata majeraha, basi angekuwa na alama za juu zaidi. Ni tishio kubwa la Arsenal linapokuja suala la mipira ya adhabu, anafunga sana.

-Jurrien Timber – 9/10; Anawania tuzo ya mchezaji bora wa msimu kwenye kikosi cha Arsenal na hakika ndiye beki wa kulia bora kwenye Ligi Kuu England kwa sasa.

-Myles Lewis-Skelly – 6/10; Amekuwa na msimu mgumu, akipoteza nafasi yake kwenye kikosi cha Arsenal, lakini bado kijana na nafasi kubwa ya kufanya vizuri kwa siku zijazo.

-Piero Hincapie – 7/10; Alianza kwa kusua kutokana na kuwa majeruhi, lakini sasa amekuwa moto, alitumika kuziba pengo la beki Gabriel wakati alipokuwa majeruhi.

EP 04

-Riccardo Calafiori – 8/10; Ni chaguo bora la Arsenal kwenye upande wa kushoto na ujio wake umemfanya Lewis-Skelly asubiri benchini. Anafunga na kuasisti.

-William Saliba – 8/10; Beki wa shoka. Arsenal inafurahi kuwa naye kwenye kikosi chake, akiunda kombinesheni matata na Gabriel na kufanya Arsenal kuwa na beki bora Ulaya.

-Declan Rice – 9/10; Ni mnyama kwenye eneo la katikati ya uwanja, huku akifanya matukio yote muhimu katika kuhakikisha Arsenal inapata matokeo bora uwanjani>

-Martin Odegaard – 7/10; Majeraha yalitaka kumtibulia, lakini baada ya kurudi uwanjani kiungo huyo ameonyesha ubora mkubwa na kuifanya Arsenal kung'ang'ania matawi ya juu.

-Martin Zubimendi – 8/10; Moja ya usajili bora kabisa kweye dirisha lililopita ulionaswa kwenye Ligi Kuu England na ujio wake unaipa timu hiyo nguvu ya ziada.

-Mikel Merino – 7/10; Kama ilivyokuwa msimu uliopita, yupo kwenye kiwango bora kabisa akifanya vyema anapewa majukumu ya kuongoza safu ya ushambuliaji. Shujaa asiyeimbwa.

Bukayo Saka – 7/10; Kuna vitu vitamu kutoka kwake, licha ya kwamba amekuwa na kiwango kilichoshuka kidogo zaidi katika msimu huu ukilinganisha na misimu iliyopita.

ARS 01
ARS 01

Wachezaji wengine

Kwa michango ya mastaa wa Arsenal na alama zake, ambapo Eberechi Eze alipata 6/10, Gabriel Jesus – 6/10, Gabriel Martinelli – 7/10, Leandro Trossard – 8/10, Max Dowman – 6/10, Noni Madueke – 7/10, Viktor Gyokeres – 5/10, Christian Norgaard – 5/10, Ethan Nwaneri – 5/10 huku Kai Havertz akiwa hajapewa alama yoyote kwa sababu hakucheza.