Mclaren safi, bado Norris

Muktasari:
- Oscar Piastri alifanikiwa kuibuka mshindi wa mbio hizo na kumfanya kuvuna pointi nyingi zaidi ya Max Verstappen tangu mbio za Monaco mapema mwaka huu ambazo ni 144 dhidi ya zile 142 za Verstappen anayeongoza kwa ujumla.
MIAKA miwili na nusu imetosha kwa kampuni ya McLaren kuvunja utawala wa kampuni ya Red Bull kukalia usukani kwa muda mrefu bila kushushwa, baada ya mbio za Baku nchini Arzebaijan Jumapili iliyopita.
Oscar Piastri alifanikiwa kuibuka mshindi wa mbio hizo na kumfanya kuvuna pointi nyingi zaidi ya Max Verstappen tangu mbio za Monaco mapema mwaka huu ambazo ni 144 dhidi ya zile 142 za Verstappen anayeongoza kwa ujumla.
Verstappen ambaye ameshinda mbio saba tofauti mwaka huu, amefikisha mbio saba mfululizo bila kushinda kiasi cha kuweka rehani ubingwa wake wa mbio hizo mbele ya Lando Norris wa McLaren anayemfuatia.
Norris ana nafasi kubwa ya kumvua taji Verstappen kutokana na kusuasua kwake kutoshinda mbio mfululizo baada ya kampuni yake kuwa ya kwanza kuwaangusha kwenye msimamo Red Bull.