Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbeumo aende, abaki freshi tu

MBUEMO (1)

Muktasari:

  • Fowadi huyo amekuwa na msimu bora kabisa kwenye kikosi hicho cha London Magharibi, akiwa amefunga mabao 19 kwenye Ligi Kuu England, huku pacha mwenzake pia kwenye safu hiyo ya ushambuliaji Yoane Wissa, naye kuwa kwenye kiwango bora.

LONDON, ENGLAND: KOCHA wa Brentford, Thomas Frank ameshindwa kufuta uwezekano wa staa wake Bryan Mbeumo kuhama kwenye dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi jambo linalowapa mzuka mkubwa Liverpool.

Fowadi huyo amekuwa na msimu bora kabisa kwenye kikosi hicho cha London Magharibi, akiwa amefunga mabao 19 kwenye Ligi Kuu England, huku pacha mwenzake pia kwenye safu hiyo ya ushambuliaji Yoane Wissa, naye kuwa kwenye kiwango bora.

Wachezaji wote hao wawili wamekuwa wakihusishwa na mpango wa kunaswa na timu nyingine dirisha la majira ya kiangazi, hasa Mbeumo.

Liverpool imetajwa kuhitaji huduma yake na kocha Frank ameonakana kufungua milango ya mchezaji huyo kuondoka, aliposema: “Amekuwa mchezaji mahiri. Kwangu mimi ilikuwa furaha kubwa kufanya naye kazi kwa miaka sita na nimekuwa nikimwona akikua tangu utoto, nadhani alikuwa na umri wa miaka 19.

“Siku zote nilifahamu kwamba ni mfungaji mahiri. Na sasa amekuwa akidumu kwa muda mrefu kwenye kazi hiyo. Namna pia anavyotuliza hali ya mchezo ni nzuri. Yupo vizuri.”

Alipoulizwa kama ataendelea kuwa mchezaji wa Brentford hadi msimu ujao, Frank alijibu: “Ngoja tuone. Tunampenda. Namtazama kila siku, amekuwa akicheza akiwa na tabasamu. Anapenda kuwa mchezaji wa Brentford, lakini ngoja tuone.”