Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sasa ngoma ni Hamisa Mobetto dhidi ya Pep Guardiola!

MOBETO Pict

Muktasari:

  • Mambo kibao yalisemwa na wadau mitandaoni baada ya tukio hilo haswa msanii huyo alipoonekana kwenye video akirudi nyumbani kwake tofauti na wengi walivyotarajia kwamba angekwea nae pipa palepale.

SIKU CHACHE zilizopita Hamisa, Miss XXL After School Bash 2010, alionekana Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), akimuaga Aziz Ki.

Mambo kibao yalisemwa na wadau mitandaoni baada ya tukio hilo haswa msanii huyo alipoonekana kwenye video akirudi nyumbani kwake tofauti na wengi walivyotarajia kwamba angekwea nae pipa palepale.

 Hatua hii inakuja takribani miezi mitatu tangu wawili hao kufunga ndoa iliyoangaziwa sana na mitandao pamoja na vyombo vya habari kutokana na nguvu yao ya ushawishi inayotokana na umahiri wa kazi zao katika sanaa na michezo Tanzania na Afrika. 

Ikumbukwe mastaa hao walithibitisha kuchumbiana Desemba 10, 2024 ambapo ilikuwa ni siku ya kuzaliwa Hamisa, mrembo huyu aliposti picha yake Instagram ikiwa imepambwa na kalenda na ndipo ikathibitika kuwa tayari yeye na Aziz Ki ni wachumba.

Sasa basi. Zimebaki siku 22 kabla ya kuanza kwa michuano mipya ya FIFA ya Kombe la Dunia la Klabu 2025 itakayofanyika Marekani, huku Hamisa Mobetto akitupa karata yake ya kwanza dhidi ya Manchester City chini ya Pep Guardiola.

Ndiyo, ni Hamisa, yule mwanamitindo, muigizaji, mwanamuziki na mshawishi maarufu wa chapa kutokea Tanzania ambaye pia ni mke wa mwanasoka Aziz Ki, Mchezaji Bora (MVP) wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita.

Aziz Ki aliyejiunga na Yanga hapo Julai 2022 akitokea ASEC Mimosas ya Ivory Coast, amesajiliwa na Wydad Casablanca na tayari ameondoka nchini kujiunga na miamba hiyo ya Morocco kwa ajili ya maandalizi ya Kombe la Dunia la Klabu. 

Katika michuano hiyo itakayoanza Juni 15 hadi Julai 13 ikijumuisha klabu 32 zilizofanya vizuri katika mabara yao, Wydad wapo kundi G pamoja na Al Ain FC (UAE), Juventus FC (Italia) na Mancheaster City (England).

Baada ya ripoti kutoka kuwa Aziz Ki atajiunga na Wydad, Hamisa alienda katika ukurasa wake wa Instagram wenye wafuasi zaidi ya milioni 12, kupitia Insta Story aliposti picha ya mumewe huyo na kumtaja kama mchezaji wa dunia.

Mapema wiki hii Hamisa, Miss XXL After School Bash 2010, alionekana Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), akimuaga Aziz Ki ambaye anaenda kuandika historia nyingine kubwa zaidi katika maisha yake ya soka.

Hatua hii inakuja takribani miezi mitatu tangu wawili hao kufunga ndoa iliyoangaziwa sana na mitandao pamoja na vyombo vya habari kutokana na nguvu yao ya ushawishi inayotokana na umahiri wa kazi zao katika sanaa na michezo Tanzania na Afrika.

Ikumbukwe mastaa hao walithibitisha kuchumbiana Desemba 10, 2024 ambapo ilikuwa ni siku ya kuzaliwa Hamisa, mrembo huyu aliposti picha yake Instagram ikiwa imepambwa na kalenda na ndipo ikathibitika kuwa tayari yeye na Aziz Ki ni wachumba.

Hiyo ni baada ya Aziz Ki kutoa maoni yake kwa lugha ya Kifaransa katika picha hiyo ya Hamisa akisema; "Nakutakia maisha yenye furaha, kuwa na furaha milele na nuru, heri ya kuzaliwa mchumba." Kisha akamalizia na emoji ya busu!

Hamisa ambaye alizaliwa mwaka 1994, huko Mwanza akiwa mtoto pekee kwa mama yake, hakuwa nyuma kuujibu ujumbe huo wa Aziz Ki, naye alitumia lugha ya Kifaransa akiandika; Merci mon fiancé - akimaanisha, asante mchumba wangu." 

Tangu wamekuwa pamoja wakionyesha kushirikiana katika kazi zao, Hamisa akijitolea vya kutosha kumuunga mkono Aziz Ki katika kazi yake soka, mathalani Januari 2025 alimzawadia viatu pea tatu alivyovinunua Afrika Kusini katika duka la Puma. 

Hivyo haitakuwa ajabu endapo Hamisa ataenda Marekani kumuunga mkono Aziz Ki katika Kombe la Dunia la Klabu, uzuri si mara ya kwanza kufika katika nchi hiyo, alishaenda mara kadhaa na hata video ya wimbo wake, Tunaendana (2018) ilifanyika huko huko.

Wydad watacheza mechi ya kwanza mnamo Juni 18 dhidi ya Man City ya Guardiola, mechi ambayo bila shaka itapata watazamaji wengi kutoka Afrika na endapo Aziz Ki atapata nafasi ya kucheza, basi wazi hata hapa Bongo itajadiliwa sana.

Man City imekuwa klabu tishio na maarufu zaidi duniani chini ya kocha Mhispania Pep Guardiola ambaye alianza kukinoa kikosi hicho tangu mwaka 2016 baada ya kuachana na mabingwa wa Bundesliga, Bayern Munich.

Hamisa ana kazi moja tu kwa sasa, nayo ni kuombea mbinu za Guardiola kushindwa kufanya kazi dhidi ya Wydad ambao msimu huu hawajafanya vizuri katika Ligi Kuu ya Morocco ambapo RS Berkane imetwaa ubingwa kwa pointi zao 70 kileleni.

Pengine hii itakuwa mara ya kwanza kwa Hamisa kuiombea ushindi badala ya kipigo Wydad ambayo kwa mara ya mwisho ilipokuja nchini kuvaana na Simba katika Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) 2023/24 ilichapwa mabao 2-0.

Bila shaka ushindi huo ulimfurahisha Hamisa ambaye wakati huo alikuwa shabiki wa Simba ila sasa yupo Yanga sababu ya Aziz Ki, hivyo ni wazi pia atakuwa shabiki wa Wydad kumunga mkono mume na kibarua chake cha kwanza ni dhidi ya Man City.

Hata hivyo, Man City ambao ndio walibeba taji hilo kwa mara ya mwisho mwaka 2023 kabla ya kuanza kwa mfumo huu mpya ambao unakutanisha klabu nyingi, wana hasira baada ya msimu uliomalizika kuwaendea vibaya wakipoteza vikombe vyote.

Mara kadhaa Hamisa ameonekana uwanjani katika mechi alizocheza Aziz Ki ikiwemo ile ya Novemba 7, 2024 pale Azam Complex ambapo Yanga ilikubali kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Tabora United.

Mbaya zaidi Hamisa alishuhudia Aziz Ki akikosa mkwaju wa penalti katika mchezo huo ambao ulikuwa ni wa pili mfululizo kwa Yanga kupoteza katika Ligi Kuu Bara msimu huu baada ya hapo awali kutandikwa na Azam FC bao 1-0 lilofungwa na Gibril Sillah.