Mara paap! Vardy anakipiga La Liga

Muktasari:
- Hilo linakuja baada ya kuwapo ripoti kwamba straika Vardy amewekwa kuwa chaguo la kwanza kwenye mpango wa usajili wa kocha wa Valencia, Carlos Corberan, ambaye anasaka kwa udi na uvumba saini ya fowadi huyo gwiji wa Leicester City mwenye umri wa miaka 38.
BARCELONA, HISPANIA: STRAIKA Jamie Vardy anaripotiwa kuwekwa kwenye rada ambazo zinaweza kumpa fursa ya kwenda kukabiliana na miamba ya Hispania, Barcelona na Real Madrid kwenye LaLiga msimu ujao.
Hilo linakuja baada ya kuwapo ripoti kwamba straika Vardy amewekwa kuwa chaguo la kwanza kwenye mpango wa usajili wa kocha wa Valencia, Carlos Corberan, ambaye anasaka kwa udi na uvumba saini ya fowadi huyo gwiji wa Leicester City mwenye umri wa miaka 38.
Kocha huyo wa zamani wa West Brom Albion ya England anataka kutumia uzoefu wa Vardy na kuamini kwamba bado ana uwezo wa kwenda kufunga mabao kwenye Ligi Kuu Hispania smimu ujao wa mashindano hayo.
Vardy alifunga mabao 10 katika kikosi cha Leicester City kilichoshuka daraja msimu huu, huku mabao tisa akifunga kwenye Ligi Kuu England.
Corberan anaamini Vardy bado ana kasi ya kwenda kumsaidia katika mtindo wake wa soka la kushambulia kwa kushtukiza.
Vardy, Jumapili iliyopita alifunga bao lake la 200 kwenye kikosi cha Leicester City baada ya kuitumikia timu hiyo kwenye 500 - ikiwa ni miaka 13 yangu alipojiunga na timu hiyo kwa ada ya Pauni 1 milioni akitokea Fleetwood Town.
Mchezaji huyo aliweka wazi kwamba anataka kubaki kwenye Ligi Kuu England, lakini anaweza kufikiria pia kubadili na kwenda kwingine ikiwamo Marekani na Saudi Arabia kuendeleza kipaji chake.
Kocha Corberan alishaanza kumshawishi Vardy juu ya mpango wa kwenda kukipiga La Mestalla.
Valencia haina pesa, hivyo kumsajili Vardy ni nafuu kwao kwa sababu anapatikana bure kabisa.