Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mastraika 20 wanaolipwa kibosi England

POCHI Pict

Muktasari:

  • Katika kuvutia vipaji vya hali ya juu kabisa kwenye mchezo wa soka kwenda kucheza kwenye Ligi Kuu England, klabu zimekuwa zikitumia pesa nyingi, hasa kwenye kulipa mishahara mikubwa wachezaji hao ili wakakipige katika ligi hiyo.

LONDON, ENGLAND: LIGI Kuu England ni moja ya ligi tajiri za mchezo wa soka duniani na kuvutia wanasoka wengi matata kabisa katika mchezo huo.

Katika kuvutia vipaji vya hali ya juu kabisa kwenye mchezo wa soka kwenda kucheza kwenye Ligi Kuu England, klabu zimekuwa zikitumia pesa nyingi, hasa kwenye kulipa mishahara mikubwa wachezaji hao ili wakakipige katika ligi hiyo.

Ni kitu cha wazi kinachokubalika kwa mashabiki wengi wa soka kwamba kazi ngumu katika mchezo huo ni kutumbuliza mipira nyavuni mara nyingi mfululizo. Na hilo ndilo linalofanya klabu kutumia nguvu nyingi kupata washambuliaji wa kuongoza safu zao za mashambulizi na kuhakikisha wanawalipa pesa nyingi ili kuwavutia kwenye vikosi vyao.

Mastraika wanalipwa mishahara mikubwa kuliko wachezaji wa safu ya mabeki.

Kwenye orodha ya mastraika matata kabisa kwenye Ligi Kuu England kuna hawa hapa 20 ambao wanaokota pesa ndefu kwenye mishahara yao ya kila wiki, ikiwamo wafumania nyavuni mahiri kabisa, akiwamo Erling Haaland, Viktor Gyokeres na Gabriel Jesus. Hawa hapa mastraika wenye mishahara ya kibabe kwenye Ligi Kuu England kwa mujibu wa mtandao wa Capology na Transfermarkt.

1.Erling Haaland (Man City, Pauni 525,000 kwa wiki)

2.Omar Marmoush (Man City, Pauni 295,000 kwa wiki)

3.Alexander Isak (Liverpool, Pauni 280,000 kwa wiki)

4.Kai Havertz (Arsenal, Pauni 280,000 kwa wiki)

5.Gabriel Jesus (Arsenal, Pauni 265,000 kwa wiki)

6.Viktor Gyokeres (Arsenal, Pauni 200,000 kwa wiki)

7.Hugo Ekitike (Liverpool, Pauni 200,000 kwa wiki)

8.Benjamin Sesko (Man United, Pauni 160,000 kwa wiki)

9.Randal Kolo Muani (Tottenham, Pauni 150,000 kwa wiki)

10.Yoane Wissa (Newcastle, Pauni 140,000 kwa wiki)

11.Ollie Watkins (Aston Villa, Pauni 130,000 kwa wiki)

12.Joao Pedro (Chelsea, Pauni 125,000 kwa wiki)

13.Joshua Zirkzee (Man United, Pauni 105,000 kwa wiki)

14.Raul Jimenez (Fulham, Pauni 100,000 kwa wiki)

15.Liam Delap (Chelsea, Pauni 100,000 kwa wiki)

16.Dominic Calvert-Lewin (Everton, Pauni 100,000 kwa wiki)

17.Eddie Nketiah (Crystal Palace, Pauni 90,000 kwa wiki)

18.Niclas Fullkrug (West Ham, Pauni 90,000 kwa wiki)

19.Dominic Solanke (Tottenham, Pauni 90,000 kwa wiki)

20.Chris Wood (Nottingham Forest, Pauni 90,000 kwa wiki)