Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mashabiki wazuiwa kuingia Marekani

MASHABIKI Pict

Muktasari:

  • Idara ya Mambo ya Nje ya Marekani (State Department) ilitoa taarifa mpya Jumatano ikielekeza maafisa wa balozi kukataa maombi ya viza kutoka nchi 75 tofauti, wakati idara hiyo ikipitia upya taratibu za kuchuja na kuchunguza waombaji.

NEW YORK, MAREKANI: MASHINDANO ya Kombe la Dunia la 2026 yamekumbwa na kikwazo kingine kikubwa baada ya mashabiki kutoka mataifa 15 yanayoshiriki mashindano hayo mambo yao ya viza kusubirishwa na Marekani chini ya Donald Trump.

Idara ya Mambo ya Nje ya Marekani (State Department) ilitoa taarifa mpya Jumatano ikielekeza maafisa wa balozi kukataa maombi ya viza kutoka nchi 75 tofauti, wakati idara hiyo ikipitia upya taratibu za kuchuja na kuchunguza waombaji.

Kati ya nchi hizo 75, mataifa 15 yanayotarajiwa kushiriki katika michuano hiyo ya majira ya kiangazi mwaka huu itakayofanyika Marekani, Mexico na Canada yamehusishwa.

Timu tatu kati ya nne katika Kundi C la Scotland zimeathiriwa na sintofahamu hii ya viza na Brazil, Morocco na Haiti zote zimejumuishwa kwenye orodha hiyo mpya.

Hali hiyo inaweza kusababisha viwanja kuwa na mashabiki wachache katika mechi zote za hatua ya makundi za Scotland, zitakazochezwa Foxborough (dhidi ya Haiti na Morocco) na Miami (dhidi ya Brazil).

Algeria, Cape Verde, Colombia, Cote d'Ivoire, Misri, Ghana, Iran, Jordan, Senegal, Tunisia, Uruguay na Uzbekistan nazo ni miongoni mwa nchi nyingine zilizoathiriwa na mpango huu ulioshtua wengi.

Inatarajiwa kuwa Idara ya Mambo ya Nje itaanza kutekeleza rasmi kusitisha kwa muda usiojulikana utoaji wa viza kuanzia Januari 21, na gazeti la Daily Mail limewasiliana na FIFA kwa ufafanuzi zaidi kuhusu namna mashabiki wa mataifa hayo watakaweza kusaidiwa.

Tarifa hiyo iliyotumwa Jumatano inaelekeza maafisa wa balozi kukataa maombi ya viza ya waombaji watakaohitaji pia kutegemea misaada ya serikali pindi wanapoingia Marekani.

Maafisa pia wameagizwa kuzingatia vigezo mbalimbali kwa waombaji, ikiwemo afya, umri na uwezo wa kuzungumza Kiingereza.

“Uhamiaji kutoka nchi hizi 75 utasitishwa wakati Idara ya Mambo ya Nje ikipitia upya taratibu za kushughulikia uhamiaji ili kuzuia kuingia kwa raia wa kigeni watakaokuwa mzigo kwa Marekani."

Nchi zilizoathiriwa ni pamoja na Brazil, Morocco, Haiti, Algeria, Cape Verde, Colombia, Cote d'Ivoire, Misri, Ghana, Iran, Jordan, Senegal, Tunisia, Uruguay na Uzbekistan.

Idara ya Mambo ya Nje imesema itatoa msamaha kwa baadhi ya maombi ya viza kwa nchi hizo ingawa itakuwa ni kwa asilimia chache sana.