Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Maresca amwaminia fundi Cole Palmer

MARESCA Pict

Muktasari:

  • Staa huyo Mwingereza amekuwa kwenye kiwango bora tangu alipojiunga na Chelsea akitokea Manchester City na alikuwa mchango mkubwa wakati The Blues ilipofanikiwa kubeba taji la UEFA Conference League msimu uliopita.

LOS ANGELES, MAREKANI: KOCHA wa Chelsea, Enzo Maresca anaamini staa wa kikosi chake Cole Palmer atajipambanua miongoni mwa mastaa wakubwa kabisa kwenye soka la dunia wakati wa fainali za Kombe la Dunia la Klabu likiendelea Marekani.

Staa huyo Mwingereza amekuwa kwenye kiwango bora tangu alipojiunga na Chelsea akitokea Manchester City na alikuwa mchango mkubwa wakati The Blues ilipofanikiwa kubeba taji la UEFA Conference League msimu uliopita.

Palmer aliasisti mara mbili kubadili sura ya mchezo kwenye fainali dhidi ya Real Betis – ambapo alitajwa kuwa Mchezaji Bora wa Mechi – akionyesha ubora wake wa kubadili mchezo kwenye mechi kubwa.

Mastaa mahiri kama Lionel Messi, Harry Kane na Kylian Mbappe wapo kwenye fainali hizo za Kombe la Dunia la Klabu zinazofanyika Marekani.

Na kocha Maresca, ambaye anamfahamu Palmer tangu walipokuwa pamoja kwenye akademia ya Man City, anaamini fowadi huyo ataonyesha ubora wake kwenye fainali hizo za Marekani.

"Nilisema zaidi ya mara moja: Cole Palmer yupo pale kwenye orodha ya wachezaji bora kabisa wenye uwezo wa kufanya kitu fulani kwa nyakati fulani, kutengeneza kitu kwenye nyakati ambazo huamini."

Palmer ni tumaini kubwa la Chelsea na amejitengeneza kuwa mchezaji mkubwa tangu alipotua katika timu hiyo, ambapo amejihakikishia nafasi ya kucheza panga pangua kwenye kikosi cha kwanza kwa misimu miwili sasa.

Na hilo ndilo linalomfanya kocha Maresca aamini Palmer kuna kitu atakifanya kwenye fainali hizo na kuliweka jina lake kwenye kapu la mastaa wanaotamba katika soka la dunia kwa sasa.

Kwenye fainali za Kombe la Dunia la Klabu, Chelsea imepangwa Kundi D pamoja na timu za Flamengo, Los Angeles FC na Esperance de Tunis.