Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Antony kuzua vita kali La Liga bei yake hadharani

TETESI Pict

Muktasari:

  • Awali, ilibainishwa kwamba Man United ingekubali ofa ya Pauni 20 milioni tu kumuuza jumla mchezaji huyo anayecheza kwa mkopo Real Betis kwa sasa, lakini sasa imeelezwa ada hiyo itaweka kwenye wakati mgumu wa kuweka sawa vitabu vyao vya kifedha.

MANCHESTER United imeripotiwa kwamba itahitaji ilipwe ada ya Pauni 32.52 milioni kwenye mauzo ya winga wa Kibrazili, Antony ili kwenda sawa na kanuni ya mapato na faida endelevu ya Ligi Kuu England.

Awali, ilibainishwa kwamba Man United ingekubali ofa ya Pauni 20 milioni tu kumuuza jumla mchezaji huyo anayecheza kwa mkopo Real Betis kwa sasa, lakini sasa imeelezwa ada hiyo itaweka kwenye wakati mgumu wa kuweka sawa vitabu vyao vya kifedha.

Real Betis ipo tayari kumchukua jumla Antony baada ya kuonyesha kiwango bora kabisa kwenye kikosi chao tangu ilipomnasa kwa mkopo kwenye dirisha la Januari, huku Barcelona ikiripotiwa kupiga hesabu za kumsajili mkali huyo kutokana na kuvutiwa na alichokifanya kwenye La Liga.

Timu nyingine zinazoripotiwa kuhitaji huduma ya Antony ni Villareal na Atletico Madrid, zote zikiwa za La Liga kitu ambacho kitakwenda kuibua vita kali.


Bruno Fernandes

LICHA ya kukosa nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao, Manchester United hawana mpango wa kukubali ofa yoyote kutoka kwa timu zinazohitaji huduma ya kapteni wao Bruno Fernandes, ambaye anawindwa na vigogo mbalimbali barani Ulaya na Al-Hilal ya Saudi Arabia ambayo inahitaji kumtumia katika michuano ya Kombe la Dunia la Klabu la FIFA.


Antonio Cordero

NEWCASTLE United wanadaiwa kuwapiku Barcelona na Real Madrid katika vita ya kuiwania saini ya winga wa Malaga, Mhispania, Antonio Cordero, 18, kuelekea dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Cordero ambaye ni miongoni mwa wachezaji vijana wanaotabiriwa kufanya makubwa hapo siku za usoni, mkataba wake na Malaga unamalizika mwisho wa msimu huu.


Liam Delap

WAWAKILISHI wa mshambuliaji wa  Ipswich Town na England, Liam Delap, 22, bado wanafanya mazungumzo na Chelsea na Manchester United kuhusu uwezekano wa staa huyo kujiunga nao katika dirisha hili la majira ya kiangazi.

Delap anawindwa na vigogo hawa kutokana na kiwango bora alichoonyesha msimu huu ambapo amefunga mabao 12 katika mechi 39 za michuano yote.


Marc Guehi

TOTTENHAM ina matumaini kuwa ushindi wake wa taji la Europa League utamshawishi beki wa Crystal Palace na England, Marc Guehi, 24, kukubali ofa ya kujiunga nayo katika dirisha hili la majira ya kiangazi.

Guehi ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika Juni 30, 2026, amekuwa akihitajika na vigogo wengi barani Ulaya kutokana na kiwango bora alichooyesha tangu msimu uliopita.


Jack Grealish

MANCHESTER City na Jack Grealish wameripotiwa kufikia makubaliano ya kuachana kwenye dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi, imefichuka.

Staa huyo mwenye umri wa miaka 29 bado ana mkataba wa miaka miwili wa kuendelea kukipiga Etihad, lakini haonekani kuwa na maisha mazuri kwenye kikosi cha Man City msimu ujao na ndio maana kuna mpango wa kubadili timu.


Nuno Tavares

LAZIO inataka kuilipa Arsenal Pauni 7.5 milioni katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi kwa ajili ya kumnunua beki wa kushoto wa timu hiyo ambaye ni raia wa Ureno, Nuno Tavares. abosi wa Lazio wanataka kutoa kiasi hicho cha pesa baada ya ripoti ya kocha wao kusisitiza kwamba asajiliwe kwani ameridhishwa na kiwango alichoonyesha msimu huu ambao anacheza kwa mkopo.


Jamie Gittens

NEWCASTLE imefikia hatua nzuri katika mazungumzo yao na Borussia Dortmund kwa ajili ya kumsajili winga wa timu hiyo na England, Jamie Gittens, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi baada ya kuvutiwa na kiwango alichoonyesha msimu huu.

Mbali ya Gittens, Newcastle pia inahitaji saini ya kipa wa Dortmund, Gregor Kobel, 27.