Man United yatinga UEFA

MANCHESTER, ENGLAND. NDIO HVYO. Manchester United imetinga katika mashindano ya Ligi Mabingwa Ulaya baada ya kuichapa Chelsea mabao 4-1 usiku usiku wa kuamkia leo.

Mabao hayo yaliwekwa kimiani na Anthony Casemiro, Martial, Marcus Rashford na Bruno Fernandea aliyefunga kwa mkwaju wa penalti, buku bao la Chelsea likiwekwa kimiani na Joao Felix.

Man United ilihitaji sare au ushindi kwenye mchezo kujihakikishia nafasi ya Ligi Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Aidha katika mchezo dhidi ya Chelsea, Man United ilipata pigo baada ya Antony kuumia,  na huenda akakosa fainali ya Kombe la FA dhidi ya Manchester City utakaochezwa wikiendi ijayo.

Antony alishindwa kuendelea na mechi na kutolewa nje kwa machela huku akibubujikwa na machozi baada ya kuumia kutokana na rafu iliyosababishwa na Trevoh Chalobah.

Winga huyo aliumia wakati akijaribu kumtoka beki wa Chelsea, Chalobah lakini kwa bahati mbaya akagongana naye na kudondoka chini eneo la hatari.

Baada ya mechi hiyo kesho Man United itacheza dhidi ya Fulham katika mechi ya mwisho ya Ligi Kuu England. Man United imeishusha Newcastle hadi nafasi ya nne kwa tofauti ya pointi mbili kwenye msimamo.