Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man United haitanii dili la Ollie Watkins

WATKINS Pict

Muktasari:

  • Man United ilikuwa na matumaini ya kumsajili mshambuliaji wa Sporting Lisbon, Viktor Gyokeres, ambaye aliwahi kufanya kazi na kocha wao wa sasa Ruben Amorim, wakati akiwa Sporting Lisbon lakini imeshindikana.

MANCHESTER, ENGLAND: MANCHESTER United imeongeza juhudi zake katika kumsajili mshambuliaji wa Aston Villa na timu ya taifa ya England, Ollie Watkins katika dirisha hili.

Man United ilikuwa na matumaini ya kumsajili mshambuliaji wa Sporting Lisbon, Viktor Gyokeres, ambaye aliwahi kufanya kazi na kocha wao wa sasa Ruben Amorim, wakati akiwa Sporting Lisbon lakini imeshindikana.

Baada ya kufeli kwa dili hilo, macho ya mashetani wekundu hao yamehamia kwa Watkins, mwenye umri wa miaka 29 ambaye ndio anaonekana kuwa mshambuliaji pekee wanayeweza kumpata kwa sasa kwani hata dili la Bryan Mbeumo kutoka Brentford pia linasumbua.

Watkins alionekana kutokuwa na furaha msimu uliopita, baada ya kupoteza nafasi katika kikosi cha kwanza mbele ya Marcus Rashford (aliyekuwa kwa mkopo kutoka United) katika nusu ya pili ya msimu.

 Aston Villa ilikosa nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa katika siku ya mwisho ya msimu, baada ya kufungwa 2-0 na Man United.

Inaripotiwa kuwa Man United tayari imefanya mazungumzo ya awali na Villa kuhusu uwezekano wa kumsajili Watkins, ambaye kocha Amorim anamwona kama mshambuliaji bora wa kuongoza safu yake ya ushambuliaji kutokana na uwezo wake wa kufunga mabao.

Villa inataka takriban Pauni 60 milioni kwa ajili ya Watkins, ambaye bado ana mkataba wa miaka mitatu hadi mwaka 2028.

Man United ilikuwa tayari kumtumia Rashford katika dili la kubadilishana na Watkins, lakini Villa ilikataa na kusisitiza kuwa inataka pesa ili kumwachia Watkins.

Kikwazo kingine kwa United ni kwamba haiwezi kumpa Watkins nafasi ya kucheza michuano ya Ulaya, baada ya kufungwa na Tottenham 1-0 katika fainali ya Europa League Mei mwaka huu, hivyo inapaswa kumpa ofa nono itakayomshawishi.

Kwa sasa, Man United pia inahitaji kuuza baadhi ya wachezaji kama Rashford, Jadon Sancho, Alejandro Garnacho na Antony ili kupata fedha za usajili mpya.

Ingawa Watkins alisaini mkataba mpya wa muda mrefu na Villa Oktoba 2023, alipata tabu ya kujihakikishia nafasi ya kucheza mwaka jana kutokana na ushindani aliokutana nao kutoka kwa Jhon Duran na baadaye Rashford.

Kocha wa Villa, Unai Emery, amesema yeye ni shabiki mkubwa wa Watkins na angetamani kumuona anabaki.

“Ni mchezaji wa kipekee. Anafanya kazi kwa bidii mno, na kujitolea kwake kila siku ni jambo la kushangaza. Lengo lake kuu ni kufunga mabao, lakini pia hutoa pasi za mabao, pia hata asipofunga wala kutoa pasi, huwa anafanya kazi kwa ajili ya timu. Anafanya pressing kwa wapinzani, anajituma sana,” alisema Unai.