Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man City yazinduka kwa Southampton

Muktasari:

BAADA ya kupoteza mchezo uliopita wa Ligi Kuu England dhidi ya Manchester United, klabu ya Manchester City imezindukia kwa Southampton na kuibuka na ushindi wa mabao 5-2 ambao umewafanya kuendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa Ligi hiyo kwa tofauti ya pointi 14.


LONDON, ENGLAND

BAADA ya kupoteza mchezo uliopita wa Ligi Kuu England dhidi ya Manchester United, klabu ya Manchester City imezindukia kwa Southampton na kuibuka na ushindi wa mabao 5-2 ambao umewafanya kuendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa Ligi hiyo kwa tofauti ya pointi 14.

Ni Ilkay Gundogan aliyetupia moja, Riyad Mahrez na  Kevin de Bruyne ambao kila mmoja alitupia mabao mawili, waliorejesha wimbi la ushindi kwa vijana hao wa Pep Guardiola, ambao kabla ya kuchapwa na Manchester United walikuwa wameche michezo 28 bila ya kupoteza

Mabao ya Southampton ambao walikuwa wakicheza soka la kushambulia kwa kustukiza,la kwanza lilikuwa kwa mkwaju wa penati iliyofungwa na Ward-Prowse huku bao la pili likifungwa na  Muingereza, Che Zach  Adams.

Mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Guardiola amekiri kwamba licha ya kuibuka na ushindi mnono walikabiliana dhidi  ya timu bora,"Kwa dakika  20  hadi  25 za kwanza walikuwa bora sana. Heshima yangu ni kubwa kwa  timu ya Ralph [Hasenhuttl]."

"Tuliteseka sana kuumudu mchezo.Tulishindwa kuumiliki mchezo hasa katika kusukuma mashambulizi yetu kwa sababu walikuwa bora kwenye eneo la kiungo cha chini. Ushindi ambao tumeupata ni kwa sababu ya viwango bora vya wachezaji tulionao,"

"Mchezo ulikuwa mgumu sana lakini jambo jema kwetu ni ushindi ambao tumeupata, imebaki michezo tisa, mchezo ujao ni dhidi ya Fulham," amesema kocha huyo.