Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man City kukatwa pointi 100!

Muktasari:

  • Hukumu ya klabu hiyo ya Etihad juu ya mashtaka 115 yaliyokuwa yakiwakabili awali, ambayo yameongezeka na kufikia 130 kuhusu kufanya udanganyifu kwenye matumizi ya pesa kwenye kikosi chao juu ya usajili wa mastaa wapya iliokuwa ikifanya pamoja na mishahara iliyokuwa ikilipa kutoka kwenye vyanzo visivyoeleweka.

MANCHESTER, ENGLAND: BALAA hilo. Manchester City imeonywa kwamba huenda ikakumbana na adhabu ya kupokwa pointi hadi 100 endapo kama itakuwa na hatia ya kukiuka matumizi kwenye Ligi Kuu England.

Hukumu ya klabu hiyo ya Etihad juu ya mashtaka 115 yaliyokuwa yakiwakabili awali, ambayo yameongezeka na kufikia 130 kuhusu kufanya udanganyifu kwenye matumizi ya pesa kwenye kikosi chao juu ya usajili wa mastaa wapya iliokuwa ikifanya pamoja na mishahara iliyokuwa ikilipa kutoka kwenye vyanzo visivyoeleweka.

Mapema mwezi huu, kocha wa Man City, Pep Guardiola alifichua kwamba hukumu yao inakaribia kutoka, aliposema Februari 7, alisema: “Katika kipindi cha mwezi mmoja, nadhani hukumu itatoka.”

Kamati huru ilisikiliza kesi hiyo kati ya Septemba na Desemba mwaka jana na yenyewe ndiyo yenye nguvu ya kuamua kuipa adhabu Man City, ambayo itaona itafaa kwa ukubwa wa mashtaka hayo ikiwamo kupokwa pointi, kushushwa daraja au kuvuliwa ubingwa.

Kupokwa pointi ni adhabu iliyoonekana kuwa ni ndogo zaidi, ambayo kwa siku za karibu klabu kama za Everton na Nottingham Forest, zilikumbana na kasheshe hilo la kupokewa pointi nane na nne mtawalia kwa msimu uliopita kufuatia kukiuka vipengele vya faida endelevu kwenye Ligi Kuu. Na sasa, mtaalamu wa masuala ya kifedha kwenye soka, Kieran Maguire, alifichua adhabu inayoweza kuikumba Man City, aliposema. “Itakuwa kunyang’anywa pointi kama itakutwa na hatia. Pointi zitakazopokwa inaweza kuwa kati ya 60 hadi 100. “Kitu kingine kinachoweza kutokea ni kama bodi ya wakurugenzi ya Manchester City kama itathibitika kuwa walidanganya na kutoa taarifa zisizo za kweli kwa mamlaka, basi itakuwa ngumu kubaki kwenye vibarua vyao, kama vile kitu kilichotokea Juventus, ambapo bodi yote ililazimika kujiuzulu.”

Kwa maelezo hayo ya Maguire, bodi nzima ya klabu ya Juventus, akiwamo rais Andrea Agnelli na makamu wake Pavel Nedved walijiuzulu Novemba 2022 wakati klabu hiyo ya Italia ipokumbana na adhabu ya kupokwa pointi 15. Hilo la viongozi likitokea, hiyo ni penalti ya pointi 10. Bodi ya wakurugenzi ya Man City inawajumuisha mwenyekiti Al Mubarak, Martin Edelman, Simon Pearce, John MacBeath, Alberto Galassi na Abdulla Khouri. Klabu hiyo ya Man City imekataa kutenda kosa kwenye mashtaka hayo yote 130.