Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mambo kibao ya kuangalia Jaylen akijiunga na Sixers

Muktasari:

  • Biashara za wachezaji zinaendelea kuwa na msisimko mkubwa kuliko usajili wa wachezaji huru katika siku za mwanzo za mapumziko ya msimu wa NBA, ambapo ulikuwa juu zaidi kwa  timu hizo mbili ambazo zimekutana mara nyingi zaidi katika historia ya NBA.

PHILADELPHIA, MAREKANI: KUONGEZWA kwa nyota Jaylen Brown katika kikosi cha Philadelphia 76ers mwenye uzoefu kunaweza kuisaidia kuvuka kikwazo katika Ukanda wa Mashariki (Eastern Conference) msimu ujao, huku Boston Celtics wakionekana kuboresha safu ya ulinzi katika Ligi ya Kikapu Marekani (NBA).

Biashara za wachezaji zinaendelea kuwa na msisimko mkubwa kuliko usajili wa wachezaji huru katika siku za mwanzo za mapumziko ya msimu wa NBA, ambapo ulikuwa juu zaidi kwa  timu hizo mbili ambazo zimekutana mara nyingi zaidi katika historia ya NBA.

Biashara ya Jaylen ilikuwa ikitarajiwa kwa muda, na hatimaye ilifanyika wiki hii ambapo Boston Celtics walimuuza kwenda Philadelphia 76ers kwa kubadilishana na Paul George, pamoja na machaguo mawili ya raundi ya kwanza (first-round picks), na mawili ya raundi ya pili (second-round picks).

Kwa Celtics, huo ni mwisho wa enzi. Katika miaka 10 aliyocheza Jaylen akiwa Boston, timu hiyo iliongoza NBA kwa ushindi wa msimu wa kawaida (530) na ushindi wa mchujo (86), huku ikitwaa ubingwa wa NBA 2024.

Licha ya Jayson Tatum kukosa mechi 62 za mwanzo msimu uliopita, Celtics walimaliza wakiwa miongoni mwa timu tano bora kwa ushambuliaji na ulinzi kwa msimu wa nne mfululizo, jambo ambalo halijawahi kutokea.

Kwa 76ers, ni uboreshaji mkubwa katika nafasi za wing (namba 3 na 4), huku pia wakipata mchezaji mwenye umri mdogo zaidi, kwani Jaylen ni mdogo kwa zaidi ya miaka sita kuliko George. Pia amecheza mechi 337 za msimu wa kawaida katika miaka mitano iliyopita ikiwa ni karibu mechi 100 zaidi ya George (239), jambo linaloongeza uhakika wa upatikanaji wake.

Swali linaloulizwa ni je anaweza kuwafikisha Sixers zaidi ya nusu fainali ya kanda? Kinachoelezwa ni kwamba 76ers waliwashangaza Celtics kwa kuwaondoa katika raundi ya kwanza ya mchujo wa 2026, lakini baadaye waliondolewa na New York Knicks katika nusu fainali ya Ukanda wa Mashariki. Hiyo ndiyo hatua ambayo safari yao imeishia mara sita katika misimu tisa iliyopita.

Tangu 2017-18, timu 19 kati ya 30 za NBA zimewahi kufika fainali za kanda angalau mara moja. Philadelphia ni miongoni mwa timu ambazo hazijawahi kufika huko, licha ya kuwa na rekodi ya tano bora ya ushindi katika msimu wa kawaida kwenye kipindi hicho.

Jaylen mwenyewe ameifikisha Boston katika fainali za kanda mara sita ndani ya misimu yake 10. Takwimu zake za mchujo zimeendelea kuwa bora kama za msimu wa kawaida, na 2024 alitwaa tuzo za MVP wa Fainali za Mashariki na MVP wa Fainali za NBA. Katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, Jaylen amecheza mechi nyingi zaidi za mchujo kuliko mchezaji mwingine yeyote. Hata hivyo, ili Philadelphia wafikie hatua inayofuata, bado watamhitaji Joel Embiid kuwa fiti mwezi Aprili na Mei, mwakani.

Swali jingine linaloulizwa ni iwapo Sixers watapata nafasi bora zaidi za kufunga? Philadelphia wamekuwa na safu ya ushambuliaji iliyo chini ya wastani kwa misimu miwili iliyopita, na walifunga wastani wa alama 106.3 pekee kwa kila mashambulizi 100 walipotolewa na Knicks.

Usajili wa Jaylen ni uboreshaji wa wazi upande wa ushambuliaji. Katika misimu miwili iliyopita amekuwa na ufanisi mkubwa wa kufunga kuliko  George, licha ya kubeba jukumu kubwa zaidi la kushambulia. Anajulikana kwa kufanikiwa kutupa mitupo migumu, lakini tatizo la Philadelphia lilikuwa kubwa zaidi ya hapo. Walikuwa nafasi ya 29 kati ya timu 30 kwa ubora wa nafasi za mitupo waliyozalisha, wakitanguliwa tu na Dallas Mavericks. Kuunganishwa kwa Jaylen, Tyrese Maxey na Embiid kunaweza kuongeza ubora wa nafasi za kufunga, mradi tu watashirikiana vizuri badala ya kulazimisha mitupo migumu.

Kwa upande wake, Celtics bado wana tatizo la kushambulia karibu na kikapu, kwani kwenye misimu mitatu iliyopita, Boston wamekuwa timu inayofanya vizuri zaidi ndani ya eneo la rangi (paint). Ingawa walitwaa ubingwa 2024 kwa mtindo huo, katika misimu miwili iliyopita walimaliza pia wakiwa timu yenye kiwango cha chini zaidi cha kwenda kwenye mstari wa penalti (free throw rate).

Mara zote mbili waliondolewa mapema katika mchujo kutokana na kushindwa kushambulia kikapu mara kwa mara. Kubadilishana Jaylen na George hakutatatua tatizo hilo. Jaylen alitupia asilimia kubwa zaidi ya mitupo yake ndani ya paint na alikuwa na safari nyingi zaidi kwenye mstari wa penalti kuliko George msimu uliopita.

Usajili wa Mitchell Robinson unaweza kusaidia kuongeza presha karibu na kikapu na kuboresha mapambano ya ribaundi za kushambulia, lakini unaweza pia kushusha asilimia ya timu katika utupaji wa ‘free throw’. Kwa ujumla, biashara hii haiongezi uwiano wa ushambuliaji wa Celtics, kwani George ni mchezaji anayependelea mitupo ya mbali kuliko kupenya kuelekea kikapuni.