Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mambo 15 ya Real Madrid unayopaswa kuyafahamu

Ni kipindi cha miaka 120  ya uwepo wa klabu ya Real Madrid katika uso wa dunia na kwenye mchezo wa soka kiujumla.

Tangu ilipoanzishwa mwaka 1902 jijini Madrid, Hispania, Real Madrid imejitambulisha na kukubalika na mamilioni ya watu ulimwenguni kote kuwa ndio klabu kubwa na bora zaidi ya soka katika sayari hii.

Ukubwa na ubora huo wa Real Madrid haujatokea kwa bahati mbaya bali ni matokeo ya mafanikio ambayo imeyapata ndani na nje ya uwanja kulinganisha na klabu nyingine za soka.

Yafuatayo ni mambo 15 yanayoifanya Real Madrid kuvutia umati mkubwa wa watu duniani ambayo yamepangwa kwa namba zinazofafanua tukio au mafanikio husika.

1. Real Madrid ndio timu iliyochaguliwa kushika nafasi ya kwanza kwa ubora katika Ligi Kuu ya Hispania 'La Liga Santander'

3. Ndio klabu ya Kwanza barani Ulaya kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya mara tatu mfululizo tangu mfumo wa mashindano hayo ulipobadilishwa. Ilifanya hivyo kuanzia msimu 2016 hadi 2018.

5. Ni klabu ya pekee barani Ulaya kushinda mataji ya Ulaya mara tano mfululizo ikifanya hivyo kati ya 1956 hadi 1960 lakini pia ndio klabu pekee ya Hispania kutwaa taji la Ligi Kui nchini humo 'La Liga' mara tano mfululizo kuanzia mwaka 1986 hadi 1990.

7. Wachezaji saba tofauti wa Real Madrid wameshinda tuzo ya Ballon d'Or mara 11 ambao ni Ronaldo De Lima, Luis Figo, Kopa, Cristiano Ronaldo, Alfred Di Stefano, Fabio Cannavaro na Luka Modric.

13. Ndio klabu yenye mataji mengi ya mashindano ya Ulaya ambayo ni 13

14. Idadi ya mataji ambayo yamechukuliwa na kocha wa zamani wa Real Madrid, Miguel Minoz ambaye ndiye kocha aliyefanikiwa zaidi katika historia ya Real Madrid

35. Imeshinda mataji 35 ya La Liga  yanayoifanya iwe timu iliyotwaa ubingwa wa ligi hiyo mara nyingi zaidi.

90. Muda maarufu kwa mashabiki wa Real Madrid ambao unafahamika kuwa unageuka mwiba kwa timu watani wao.

100. Real Madrid ndio timu  iliyowahi kufikia rekodi ya kukusanya pointi 100 kwa msimu mmoja kwenye La Liga Santander ikifanya hivyo katika msimu wa 2011/2012.

121. Real Madrid ndio timu pekee iliyofunga mabao mengi zaidi katika msimu mmoja wa La Liga ambapo ilikuwa ni katika msimu wa 2011/2012 ilipofunga mabao 121.

450. Mabao yaliyofungwa na Cristiano Ronaldo katika mashindano yote yanayomfanya awe mfungaji bora wa muda wote wa Real Madrid. Kati ya mabao hayo, mabao 311 ameyafunga katika La Liga Santander.

741. Raul Gonzalez ndiye mchezaji aliyeichezea Real Madrid mechi nyingi ambazo ni 741. Kati ya hizo, mechi 550 ni za La Liga Santander.

1902. Mwaka ambao Real Madrid ilianzishwa

1947. Mwaka ambao Uwanja wa Real Madrid wa Santiago Bernabeu ulifunguliwa rasmi.

2000. Mwaka ambao Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) liliitaja Real Madrid kama klabu bora ya Karne