Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Majembe ya Man United yamerudi

Muktasari:

  • Beki huyo Mfaransa, Yoro alikosa mechi mbili zilizopita kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya enka.

MANCHESTER, ENGLAND: MANCHESTER United imeongezewa mzuka baada ya beki wao wa kati, Leny Yoro na mastaa wengine wanne kurejea kwenye kikosi wakiwa fiti kwa ajili ya kuendeleza mapambano ya kuhakikisha timu inamaliza vizuri msimu huu.

Beki huyo Mfaransa, Yoro alikosa mechi mbili zilizopita kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya enka.

Hata hivyo, sasa yupo kwenye hatua za mwisho kurejea uwanjani kukipiga baada ya kuonekana mazoezini baada ya kupita kwa mapumziko ya mechi za kimataifa. Yoro sasa anajiandaa kwa ajili ya mechi ijayo ya Ligi Kuu England na Man United inajiandaa kukipiga na Nottingham Forest, Jumanne.

Yoro si beki pekee atakayerejea kwenye kikosi cha Man United baada ya Harry Maguire naye kuwa kwenye hatua za mwisho kabisa za kujiweka kwenye utimamu mkubwa ili kurudi uwanjani.

Beki huyo Mwingereza amekuwa nje ya uwanja tangu mwanzoni mwa mwezi Machi kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya paja, lakini sasa ameonekana kupona na huenda akacheza dhidi ya Forest.

Kuna mzuka mwingine kwa Kocha Ruben Amorim kwenye safu yake ya ulinzi kutokana na kurejea kwa Luke Shaw.

Beki huyo wa kushoto amekuwa akisumbuliwa na majeraha kwa muda mrefu msimu huu na kujikuta akicheza mechi tatu tu. Lakini, sasa amerejea mazoezini na bila ya shaka atajumuishwa kwenye kikosi cha mechi hiyo ya City Ground.

Ukiachana na wakali hao wa safu ya ulinzi walirejea uwanjani, taarifa njema ni khusu makipa Altay Bayindir na Tom Heaton, ambao wote wamerejea uwanjani. Ukiachana na wachezaji majeruhi, staa wao waliyemsajili Januari, Patrick Dorgu atarejea uwanjani baada ya kutumikia adhabu yake ya mechi tatu kufuatia kadi nyekundu aliyoonyeshwa dhidi ya Ipswich Town. Man United itakipiga na Forest katikati ya wiki ijayo kabla ya kukipiga kwenye Manchester derby uwanjani Old Trafford wikiendi ijayo. Baada ya hapo, kikosi hicho cha kocha Amorim kitakwaruzana na Lyon kwenye mechi ya kwanza ya hatua ya robo fainali ya michuano ya Europa League.

Wachezaji ambao wataendelea kukosekana kwenye kikosi cha Man United ni beki wa kati Lisandro Martinez, anayesumbuliwa na maumivu ya goti na winga Amad.

Mabeki wa kati Ayden Heaven na Jonny Evans wataendelea kuwa nje ya uwanja, wakati kinda Heaven aliumia kwenye mechi ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Leicester na kocha Amorim alisema: “Tutawafanyia tathmini wiki hii. Heaven bado ni kijana mdogo na hajui namna ya kuelezea anavyojisikia, hivyo inakuwa ngumu kwetu kujua tatizo.”