Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Maguire ndani, Trent nje England

Muktasari:

  • Lakini, jambo la kushangaza kwa mashabiki wa England ni kwamba, kipa namba mbili wa kikosi hicho, Nick Pope      anayeichezea Newcastle United ameachwa, huku beki anayecheza kiungo na winga, Trent Alexander-Arnold akiachwa.

LONDON, ENGLAND: KOCHA wa timu ya taifa ya England, Thomas Tuchel, ametangaza kikosi cha wachezaji 35 wakiwemo watatu ambao hawajawahi kucheza mechi za kimataifa, huku beki wa Manchester United, Harry Maguire na kiungo Kobbie Mainoo wakirejea.

Lakini, jambo la kushangaza kwa mashabiki wa England ni kwamba, kipa namba mbili wa kikosi hicho, Nick Pope      anayeichezea Newcastle United ameachwa, huku beki anayecheza kiungo na winga, Trent Alexander-Arnold akiachwa.

Kuachwa kwa Trent siyo gumzo tu England, bali hata Hispania anakoichezea Real Madrid kwani mastaa wenzake kikosini wote wameita kukitumikia kikosi cha timu ya taifa.

Tuchel amemuita kwa mara ya kwanza kiungo wa Everton, James Garner baada ya kuvutiwa na kiwango chake chini ya kocha David Moyes, ambapo atakuwa miongoni mwa mastaa waliojumuishwa katika kikosi kwa ajili ya mechi za kirafiki dhidi ya Uruguay na Japan zitakazochezwa kwenye Uwanja wa Wembley.

Pia, kiungo wa Real Madrid, Jude Bellingham ameitwa licha ya kuwa nje ya uwanja tangu Februari 1 kutokana na majeraha ya misuli, lakini alisafiri na timu yake kwenye ushindi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Manchester City, lakini hakucheza.

Hii ni nafasi ya mwisho kwa Tuchel kuwapima wachezaji wake kabla ya kutangaza kikosi kamili kitakachocheza fainali za Kombe la Dunia 2026 zitakazofanyika Marekani, Canada na Mexico.

Maguire, ambaye ana mechi 64 za kimataifa hajaichezea England tangu Septemba 2024, lakini kurejea kwa kiwango chake kumeongeza nafasi yake ya kujumuishwa kwenye kikosi cha Kombe la Dunia.

Mshambuliaji wa Leeds United, Dominic Calvert-Lewin amerejea kwa mara ya kwanza tangu 2021 baada ya kufunga mabao 10 ya Ligi Kuu England msimu huu, huku beki wa Newcastle United, Lewis Hall naye akiitwa ili kuimarisha beki ya kushoto.

KIKOSI KAMILI

Makipa: Dean Henderson, Jordan Pickford, Aaron Ramsdale, Jason Steele, James Trafford

Mabeki: Dan Burn, Marc Guehi, Lewis Hall, Ezri Konsa, Tino Livramento, Harry Maguire, Nico O’Reilly, Jarell Quansah, Djed Spence, John Stones, Fikayo Tomori

Viungo: Elliot Anderson, Jude Bellingham, James Garner, Jordan Henderson, Kobbie Mainoo, Declan Rice, Morgan Rogers, Adam Wharton

Washambuliaji: Jarrod Bowen, Dominic Calvert-Lewin, Eberechi Eze, Phil Foden, Anthony Gordon, Harry Kane, Noni Madueke, Cole Palmer, Marcus Rashford, Bukayo Saka, Dominic Solanke