Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Morocco yaichapa Canada chuma tatu, yaandika historia

Muktasari:

  • Ushindi huo umeifanya Morocco kuendeleza rekodi ya kutopoteza mechi 10 mfululizo huku Canada ikimaliza safari yake ya kihistoria kwenye michuano hiyo na kuwa mwenyeji wa kwanza kuondolewa.

Morocco imekuwa timu ya kwanza kufuzu hatua ya robo fainali ya Kombe la Dunia 2026 baada ya kuwachapa wenyeji wenza Canada mabao 3-0 katika mchezo wa hatua ya 16 bora uliochezwa leo Jumamosi, Julai 4, 2026.

Ushindi huo umeifanya Morocco kuendeleza rekodi ya kutopoteza mechi 10 mfululizo huku Canada ikimaliza safari yake ya kihistoria kwenye michuano hiyo na kuwa mwenyeji wa kwanza kuondolewa.

Licha ya kupoteza mchezo, Canada ndiyo iliyoanza kwa kasi na kutengeneza nafasi nzuri ya kufunga ndani ya dakika 15 za mwanzo. Tani Oluwaseyi alijikuta ana kwa ana na kipa Yassine Bounou, lakini mlinda mlango huyo wa Morocco aliokoa kwa ustadi mkubwa.

Canada iliendelea kuonyesha nia ya kushambulia katika kipindi cha kwanza, huku Alistair Johnston akipoteza nafasi nyingine ya wazi baada ya kichwa chake kuzuiwa na safu ya ulinzi ya Morocco.

Kwa upande wa Morocco, ilishindwa kutengeneza nafasi nyingi za hatari katika dakika 45 za kwanza, huku jaribio pekee likiwa shuti la mbali la Soufiane Rahimi lililodakwa kirahisi na kipa Maxime Crépeau.

Hata hivyo, Morocco ilirejea kipindi cha pili ikiwa imebadilika kabisa na kufanikiwa kupata bao la kuongoza dakika tano baada ya mapumziko.

Achraf Hakimi alipiga mpira wa adhabu uliomkuta Azzedine Ounahi, ambaye hakufanya makosa na kuuweka mpira wavuni.

Bao hilo lilibadilisha mwelekeo wa mchezo, Morocco ikaanza kutawala zaidi huku Canada ikilazimika kusukuma wachezaji wengi mbele kutafuta bao la kusawazisha.

Canada ilipata nafasi nzuri kupitia mpira wa adhabu wa Jonathan David, lakini shuti lake lilipaa juu ya lango kabla ya Tajon Buchanan kulazimisha Bounou kufanya moja ya sevu bora za mchezo kwa shuti kali la mbali.

Wakati Canada ikiendelea kushambulia, Morocco ilitumia mwanya ilioupata kwa shambulizi la kushtukiza. Brahim Diaz alikokota mpira upande wa kulia kabla ya kumpasia Ounahi ambaye alipiga shuti lililojaa moja kwa moja wavunu na kufunga bao la pili.

Dakika za nyongeza, Soufiane Rahimi alihitimisha ushindi huo kwa kufunga bao la tatu na kuifanya Morocco ishinde kwa mabao 3-0 mbele ya wenyeji hao.

Kwa ushindi huo, Morocco imeandika historia kwa kuwa taifa la kwanza kutoka Afrika kufuzu robo fainali ya Kombe la Dunia mara mbili.

Mafanikio hayo yanaendeleza rekodi yao nzuri baada ya kufika nusu fainali katika Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar ambapo ilikwenda hadi nusu fainali na kumaliza nafasi ya nne.

Kwa upande wa Canada, licha ya kuondolewa, timu hiyo imeandika historia kwa kufuzu hatua ya 16 bora ya Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza, lakini ilishindwa kuhimili ubora wa Morocco katika kipindi cha pili.

Kiungo Azzedine Ounahi alichaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Mechi baada ya kufunga mabao mawili yaliyoihakikishia Morocco ushindi na tiketi ya kucheza robo fainali.

Sasa Morocco itakutana na mshindi wa mchezo kati ya Ufaransa na Paraguay katika hatua ya robo fainali.