Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

MAGIC JOHNSON: Kinara wa asisti fainali NBA

JOHNSON Pict

Muktasari:

  • Katika NBA, hasa kwenye hatua ya fainali kila mpira unaopitishwa kwa usahihi na kusababisha pointi ni mchango mkubwa unaoweza kuamua hatima ya taji.

INDIANA, MAREKANI: KATIKA ulimwengu wa mpira wa kikapu kuna usemi maarufu unaosema “mpira unapita haraka kuliko mchezaji.” Hii inaashiria umuhimu wa pasi sahihi katika kuongoza timu kupata ushindi.

Katika NBA, hasa kwenye hatua ya fainali kila mpira unaopitishwa kwa usahihi na kusababisha pointi ni mchango mkubwa unaoweza kuamua hatima ya taji.

Wakati wengi huangalia wachezaji wanaofunga pointi nyingi kuna kundi la wachezaji ambao kazi yao ni kutengeneza nafasi, kusoma mchezo na kuhakikisha mpira unafika kwa anayestahili kufunga. Hawa ndio ‘watawala’ wa asisti.

Katika historia ya fainali za NBA kuna wachezaji wachache  wametoa asisti nyingi kwenye mechi moja. Kinara wao ni Magic Johnson ambaye jina lake linaonekana mara nne kati ya tano bora.

Akiwa mmoja wa waongoza mashambulizi bora ‘point guards’ wa muda wote, Johnson alitawala mechi kwa akili zaidi ya nguvu. Hii hapa ni orodha ya wachezaji waliofungua milango kwa wenzao na kuweka historia ya kutoa asisti  nyingi zaidi katika mechi moja ya fainali ya NBA.


1. MAGIC JOHNSON (21)

Katika msimu wa 1983-84, Magic Johnson alionyesha kiwango cha juu kwa kutoa wastani wa asisti 13.1 kwa mechi akiongoza ligi na kumaliza nafasi ya tatu katika kura za MVP. Los Angeles Lakers ilitinga fainali na ikakutana na mahasimu wake wa kihistoria, Boston Celtics.

Katika Game 3, Magic aliandika rekodi kwa kutoa asisti 21 rekodi ambayo haijavunjwa hadi leo kwenye mechi za fainali ya NBA. Pasi zake zilichangia Lakers kushinda mchezo ingawa walishindwa kutwaa ubingwa baada ya kupoteza Game 7.

JOHN 01

2. MAGIC JOHNSON (20)

Miaka saba baada ya rekodi yake ya kwanza, Johnson alirejea tena kwenye orodha. Katika msimu wa 1990-91 alitoa wastani wa asisti 12.5 na pointi 19.4 akimaliza nafasi ya pili kwenye kura za MVP.

Lakers ilifika fainali ikikutana na Chicago Bulls iliyokuwa na Michael Jordan aliyekuwa katika kilele cha uwezo. Katika Game 5 licha ya ushindani, Magic alionyesha ustadi wa hali ya juu kwa kutoa asisti 20 na kufanikisha kuongeza pointi 16 na rebounds 11. Licha ya kiwango  bora, Lakers ilipoteza mchezo na Bulls ikatwaa ubingwa.

JOHN 02

3. MAGIC JOHNSON (20)

Mwaka 1987 ulikuwa wa mafanikio makubwa kwa Johnson, kwani alipata tuzo ya kwanza ya MVP baada ya kutoa wastani wa asisti 12.2 na kufunga wastani wa pointi 23.9 kwa mchezo. Lakers ilipambana tena na Celtics katika fainali. Katika Game 2, Johnson alitoa asisti 20 akiongoza Lakers kushinda mchezo na kuchukua uongozi wa 2-0 kwenye mfululizo wa michezo. Hatimaye Lakers ilitwaa ubingwa kwa ushindi wa michezo 4-2 huku akitajwa kuwa MVP wa fainali.

JOHN 03

4. WALT FRAZIER (19)

Walt Frazier, mmoja wa ‘guards’ mahiri wa enzi zake aliweka historia 1970 Akiwa kwenye msimu wake wa tatu NBA ambapo alitupia wastani wa asisti 8.2 kiwango cha juu zaidi katika maisha yake ya uchezaji.

Katika Game 7 ya fainali dhidi ya Lakers, Frazier alicheza mechi ya maisha yake kwa kufunga pointi 36 na kutoa asisti 19. Aliiongoza New York Knicks kutwaa ubingwa wa kwanza. Huo ulikuwa msimu bora zaidi kwake binafsi akimaliza nafasi ya nne katika kura za MVP.

JOHN 04

5. MAGIC JOHNSON (19)

Katika Game 6 ya fainali 1987, Johnson aliisaidia Lakers kufunga mfululizo dhidi ya Boston Celtics kwa kutoa asisti 19. Mwaka mmoja baadaye aliirudia rekodi hiyo  dhidi ya Detroit Pistons katika Game 6 ya fainali 1988.

Lakers ilikuwa nyuma kwa michezo 3-2 na ushindi huo ulikuwa muhimu ambapo ilishinda Game 7 na kutwaa ubingwa wa pili mfululizo ikiwa ni taji la tano na la mwisho kwa kwake katika maisha ya NBA.