Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ayoub Lakred, Simba kuna kitu

AYOUB Pict

Muktasari:

  • Lakred siyo mchezaji mpya, bali ni yuleyule raia wa Morocco aliyewahi kuwa nguzo muhimu katika kikosi cha Wekundu wa Msimbazi kabla majeraha hayajamtupa nje kwa zaidi ya miezi mitano.

MSIMBAZI kuna kitu kinaendelea chini kwa chini wakati macho ya mashabiki wa Simba yakielekezwa kwenye sakata la dabi, nyuma ya pazia jina la kipa Ayoub Lakred limeanza kuzungumziwa kwenye korido za uongozi wa klabu hiyo katika hesabu za kuboresha kikosi msimu ujao.

Lakred siyo mchezaji mpya, bali ni yuleyule raia wa Morocco aliyewahi kuwa nguzo muhimu katika kikosi cha Wekundu wa Msimbazi kabla majeraha hayajamtupa nje kwa zaidi ya miezi mitano.


Ni kama filamu vile. Lakred ambaye alionekana hana nafasi tena ndani ya Simba, hivi sasa amerudi kwa kasi baada ya taarifa kutoka ndani ya klabu kudokeza kuwa uongozi uko mbioni kumrudishia mikoba na hata kumpa mkataba mpya mara tu ule wa sasa utakapoisha.

Na sababu ya mabadiliko hayo ni Moussa Camara aliyesajiliwa kwa dharura kuziba pengo lililoachwa na kipa huyo aliyekuwa ameumia.

Camara kwa msimu wa kwanza amefanya mambo makubwa akiiongoza Simba hadi fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika akiwa na ‘clean sheet’ sita katika mechi 14 na 17 za Ligi Kuu akimzidi mbili Djigui Diarra wa Yanga mwenye 15.

Lakini, mafanikio hayo hayajazima minong’ono ya kutoridhishwa naye kwa baadhi ya viongozi wa Simba.

Makosa ya hapa na pale pamoja na masuala ya kinidhamu nje ya uwanja yameanza kutia doa mustakabali wa Camara ndani ya klabu hiyo. Hali hiyo ndiyo inayotajwa kufungua milango ya Lakred kurejea kikosini kama kipa namba moja.

Kama Simba ingefanya uamuzi wa haraka, Lakred asingekuwa anatazamwa tena Msimbazi. Klabu ilishaanza mchakato wa kuvunja mkataba baada ya jeraha lake kubwa lililompoteza kabla hata msimu mpya haujaanza.

Hata hivyo, kipengele cha kifedha kwenye mkataba wake kiliilazimisha Simba kuachana na mpango huo kutokana na kiasi kikubwa cha fedha ambacho ingetakiwa kumlipa.

Kwa busara, ikaamua kumbakiza hadi mkataba wake umalizike, ingawa jina lake liliondolewa kwenye orodha ya wachezaji msimu huu.

Na sasa, kama hadithi ya shujaa anayerejea vitani, Ayoub amekuwa akifanya mazoezi kikamilifu na inaripotiwa kuwa yuko fiti kwa asilimia kubwa. Benchi la ufundi la Simba, likiongozwa na Fadlu Davids limebariki mpango wa kurejeshwa kwake kwenye kikosi cha kwanza.

Hii ni baada ya kubaini kuwa kipa huyo bado ana kiwango cha juu na anaweza kuwa suluhisho katika eneo la lango.

“Mabosi wameanza mazungumzo naye ili asalie kikosini jumla, kwani mkataba wake unafikia mwishoni, lakini kitakachoamuliwa kinasubiri baada ya kumalizika kwa ligi, kwani Lakred hajawahi kuondoka Simba licha ya kwamba hakuwa anacheza, alikuwa akilipwa kama kawaida,” kilisema chanzo kutoka ndani ya Simba.

Sambamba na mpango wa kumrudisha Lakred, klabu hiyo pia imeanza kusaka kipa mzawa mwenye uwezo mkubwa wa kumpa changamoto ya kweli.

 Na jina linalotajwa zaidi kwa sasa ni la Yakoub Suleiman, kipa wa JKT Tanzania na timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.

Yakoub hajaruhusu bao katika mechi nane za Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.

Uwezo wake wa kupangua mashambulizi, kusoma mchezo na kutawala eneo la hatari umevutia macho ya mabosi wa Simba wanaotaka kujenga safu ya ulinzi imara zaidi kwa ajili ya msimu ujao.

Kikosi cha Yakoub kinakamata nafasi ya sita katika msimamo wa Ligi Kuu Bara.