Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Madrid yawasilisha maombi Liverpool dili la Trent

Tetesi Pict
Tetesi Pict

Muktasari:

  • Mpango wa Madrid ni kuhakikisha staa huyu wa kimataifa wa England anatua katika timu yao na ili kuwa na uhakika wanataka kumaliza kazi Januari kwa kumpa mkataba wa awali.

RASMI Real Madrid  imeitaarifu Liverpool kwamba inataka kuzungumza na beki wao wa pembeni Trent Alexander Arnold ambaye inaweza kumsainisha mkataba wa awali ifikapo Januari.

Mpango wa Madrid ni kuhakikisha staa huyu wa kimataifa wa England anatua katika timu yao na ili kuwa na uhakika wanataka kumaliza kazi Januari kwa kumpa mkataba wa awali.

Trent mwenye umri wa miaka 26, hadi sasa hajaanza mazungumzo ya mkataba mpya na Liverpool hali inayozidi kuongeza asilimia za kutua Madrid mwisho wa msimu.

Tangu kuanza kwa msimu huu beki huyu amecheza mechi 15 za michuano yote na kutoa asisti mbili.

Madrid inadaiwa pia kumtumia staa wao Jude Bellingham kama sehemu ya ushawishi ili kuhakikisha Trent anakubali kutua kwani wawili hao ni marafiki.


Wakati huo huo straika wa Ipswich Town, Liam Delap amezidi kuzichanganya timu mbalimbali England zinazohitaji huduma yake dirisha lijalo. Delap mwenye umri wa miaka 21, ameonyesha kiwango bora tangu kuanza kwa msimu huu na amecheza mechi 12 za michuano yote na kufunga mabao sita. Mkataba wake unamalizika mwaka 2029 na kuna kila dalili akatua katika moja ya vigogo England na zinatajwa Chelsea na Manchester City ndizo zinaongoza kumwania nyota huyu.


TOTTENHAM imepanga kumsajili beki wa kulia wa RB Leipzig na Uholanzi, Lutsharel Geertruida, 24, ili akawe mbadala wa Pedro Porro anayeweza kutua Real Madrid dirisha lijalo. Awali ilielezwa Spurs haina mpango wa kumuuza staa huyo lakini mambo yamebadilika baada ya Porro mwenyewe kuwasilisha maombi ya kutaka kuondoka. Madrid inataka kumsajili fundi huyu kutokana na mapungufu iliyonayo katika eneo lao la beki kutokana na idadi kubwa ya majeruhi.


WOLVES haitaki kumuuza mshambuliaji wao raia wa Brazil, Matheus Cunha, 25, ambaye anawindwa na timu mbalimbali barani Ulaya ikiwemo Manchester United na Tottenham. Katika kuhakikisha staa huyo anabaki, Wolves inataka kumpa ofa ya mkataba mpya ambao utakuwa na nyongeza ya mshahara na bonasi ukilinganisha na kile ambacho anakipata kwa sasa.


CHELSEA inaongoza katika harakati za kuiwania saini ya beki wa pembeni wa Lecce na Denmark, Patrick Dorgu, 20, katika dirisha lijalo la majira ya baridi. Kwa mujibu wa tovuti ya Caught Offside, Lecce inahitaji kiasi kisichopungua Pauni 50 milioni ili kumuuza staa huyo. Tangu kuanza kwa msimu huu Dorgu amecheza mechi 14 za michuano yote na kuna kila dalili akatua darajani dirisha dogo.


BARCELONA inatarajiwa kutuma ofa Wolves ili kuipata saini ya beki wao wa kushoto, Hugo Bueno, 22, ambaye kwa sasa anaichezea kwa mkopo Feyenoord na ripoti zinaeleza wawakilishi wa Barca wapo Uholanzi kwa muda sasa kufuatilia maendeleo ya fundi huyu. Bueno mwenye umri wa miaka 22, mkataba wake wa sasa na Wolves unatarajiwa kumalizika mwaka 2028.


LIVERPOOL inatajwa inaongoza katika mchakato wa kuiwania saini ya beki  wa kushoto wa Fulham, Antonee Robinson, 27, ambaye ameonyesha kiwango bora tangu kuanza kwa msimu huu. Timu hizi zinataka kumsajili dirisha la majira ya baridi lakini Fulham haionekani kuwa na mpango wa kumuuza kwa wakati huo. Mkataba wa Robinson unatarajiwa kumalizika mwaka 2028.


EVERTON inapambana kumbakisha staa wao, Dominic Clevert Lewin dirisha lijalo licha ya kuwepo kwa timu zinazomhitaji. Lewin mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu huu na ifikapo Januari ataruhusiwa kusaini mkataba wa awali na timu ya nje ya England. Msimu huu amecheza mechi 12 za michuano yote na kufunga mabao mawili.