Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pogba: Monaco? Bado sijasaini

POGBA Pict

Muktasari:

  • Mfaransa huyo amekuwa hana timu kwa karibu miaka miwili baada ya kukutwa na hatia kwenye matumizi ya dawa zinazopigwa marufuku michezoni, lakini sasa anatafuta timu mpya.

MONACO, UFARANSA: KIUNGO wa boli, Paul Pogba amesema tena kwa msisitizo “sijasaini chochote” wakati huu ikiripotiwa kuwa staa huyo wa zamni wa Manchester United atajiunga na Monaco.

Mfaransa huyo amekuwa hana timu kwa karibu miaka miwili baada ya kukutwa na hatia kwenye matumizi ya dawa zinazopigwa marufuku michezoni, lakini sasa anatafuta timu mpya.

Timu yake ya mwisho kuichezea ilikuwa Juventus, lakini miamba hiyo ya Italia haina mpango wa kumsajili kwa mara ya tatu. Pogba sasa akiwa kwenye umri wa miaka 30, lakini amethibitisha ubora wake kwa kipindi chote alichokuwa uwanjani, licha ya kwamba amekuwa na tatizo la kucheza kwenye kiwango cha juu kwa muda mrefu.

Monaco, ambayo ipo kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, ipo tayari kumchukua mshindi huyo wa Kombe la Dunia na Le Parisien iliripoti wiki iliyopita kwamba Pogba anajiandaa kujiunga na miamba hiyo ya Ligue 1 kwa mkataba wa miaka miwili. Hilo litakuwa ongezeko bora kwenye kikosi cha Monaco kwa kumpa Pogba fursa ya kurudi kucheza soka kwao tangu alipoondoka Le Harve mwaka  2009.

Hata hivyo, mchezaji mwenyewe ameibuka na kufichua ukweli juu ya ishu hiyo ya kwenda Riviera.

Pogba alisema kwenye kipindi la La Casa del Kun, redio mtandao ya straika wa zamani wa Manchester City na Argentina, Sergio Aguero alisema: “Sijasaini chochote, lakini kuna wanaonihitaji. Ngoja tuone.”

Pogba pia anahusishwa na mpango wa kwenda Amerika Kusini kukipiga kwenye miamba ya Argentina, Boca Juniors, aliposema: “Kwenye maisha, huwezi kujua. Nilipenda kuona watu wanaokwenda kuitazama Boca, wanavutia.”

Kiwango cha soka la Pogba bado hakijafikia kwenye ukomo wake kama watu walivyomtarajia. Alionyesha kiwango bora wakati alipoondoka Manchester kwa mara ya kwanza kung’ara Juventus, jambo ambalo lilisababisha miamba hiyo ya zamani ya Old Trafford kulipa ada kubwa kumrudisha kwenye kikosi chao wakati walipokuwa chini ya kocha Jose Mourinho.

Hata hivyo, aliporudi Man United kiwango chake hakikuwa kwenye ubora ule na baada ya hapo alirudi Juventus kwa uhamisho wa bure, kabla ya kukutwa na tatizo hilo la matumizi ya dawa haramu na kuingia kwenye kifungo cha kisoka.