Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Madrid yapanga jambo dili la Alphonso Davies

tetesi Pict
tetesi Pict

Muktasari:

  • Madrid kwa sasa inataka kuwekeza nguvu zaidi  kwenye dili la beki wa Liverpool, Trent Alexander Arnold ambaye mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu.

REAL Madrid huenda ikaachana na mpango wa kutaka kumsajili beki wa kushoto wa Bayern Munich na Canada, Alphonso Davies,  baada ya kuona staa huyo anachelewa kufanya uamuzi kama atajiunga nao au atabakia Bayern.

Madrid kwa sasa inataka kuwekeza nguvu zaidi  kwenye dili la beki wa Liverpool, Trent Alexander Arnold ambaye mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu.

Davies ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu,  amekuwa katika kiwango bora kwa muda mrefu na tangu kuanza kwa msimu amecheza mechi 20 za michuano yote.

Awali Madrid ilikuwa ikipambana na kutaka kumpata hata dirisha la majira ya baridi mwakani lakini presha hiyo kwa sasa imepungua baada ya mastaa wao waliokuwa majeruhi katika eneo lao la ulinzi, Dani Carvajal, Eder Militao na Lucas Vazquez kurejea.


LIVERPOOL inamwangalia mshambuliaji wa Brighton, Joao Pedro kama mmoja wa mastaa inaohitaji kuwasajili katika dirisha la majira ya kiangazi mwakani. Joao mwenye umri wa miaka 23, mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2028. Msimu huu amecheza mechi tisa za michuano yote na kufunga mabao manne na ameonyesha kiwango bora kilichowavutia vigogo wa Majogoo hao na kuamua kumfungia kazi mwisho wa msimu huu.



MANCHESTER United inataka ofa ya Pauni 40 milioni kutoka kwa timu yoyote itakayohitaji huduma ya mshambuliaji wao Marcus Rashford katika dirisha lijalo. Hata hivyo, hadi sasa hakuna ofa yoyote iliyowasilishwa na timu yoyote kwa ajili ya kumsajili. Mkataba wa Rashford unamalizika mwaka 2028. Msimu huu amecheza mechi 23 za michuano yote na kufunga mabao saba na anashutumiwa kushuka kiwango licha ya umri wake bado unaruhusu kuwa katika ubora.



MANCHESTER City imefikia hatua nzuri katika harakati zao za kutaka kumsajili winga wa Bayer Leverkusen, Florian Wirtz, ambaye inataka kuwatoa mastaa wao, Oscar Bobb, 21, au James McAtee, 22, kama sehemu ya ofa. Mkataba wa sasa wa Wirtz unatarajiwa kumalizika mwaka 2027.Timu nyingi zilitamani kumsajili tangu dirisha lililopita la majira ya kiangazi lakini ilishindikana.


MANCHESTER United imemuweka katika orodha ya mastaa inaohitaji kuwasajili dirisha lijalo straika wa Juventus na Serbia, Dusan Vlahovic, 24. Dusan ambaye mkataba wake unamalizika mwaka 2026, msimu huu amecheza mechi 18 za michuano yote na kufunga mabao 10. Mbali ya Man United huduma yake pia inahitajika na Arsenal na kiwango bora ndicho kilichozishawishi klabu hizo kumsaka.


Bayer Leverkusen inafanya kazi ya ziada kuhakikisha inaipata huduma ya  kiungo wa  Real Madrid na Uturuki, Arda Guler, 19, katika dirisha lijalo la majira ya baridi kwa mkopo wa nusu msimu. Arda ambaye hapati nafasi ya kutosha kikosi cha kwanza cha Madrid msimu huu amekuwa akitajwa kuondoka na hivi karibuni kocha Carlo Ancelotti alisisitiza kuwa bado ana mipango naye.


WOLVES ipo kwenye hatua za mwisho kumsainisha mkataba mpya beki wao wa kulia raia wa Ureno, Nelson Semedo, 31, ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu. Ripoti zinadai mabosi wa Wolves wanahitaji kumuongeza Semedo mkataba mpya baada ya kuona kuna baadhi ya timu zinamnyemelea.


JUVENTUS inapambana kumsajili kwa mkopo kiungo wa Chelsea na Italia, Cesare Casadei, 21, ambaye pia anahusishwa na Monza. Casere anahusishwa kuondoka kwa mkopo kwa sababu hapati nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza cha Chelsea na msimu huu amecheza mechi tano za michuano yote. Mkataba wake unamalizika mwaka 2028.