Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Luis Enrique, Man United kuna jambo linakuja

ENRIQUE

Muktasari:

  • Kocha huyo Mhispania ametajwa kama mrithi anayeweza kuchukua mikoba ya Michael Carrick, ambaye kwa sasa ana mkataba na Man United hadi mwisho wa msimu huu.

MANCHESTER, ENGLAND: VYANZO vya kuaminika vimeweka wazi juu ya wapi kocha wa PSG, Luis Enrique, anaweza kufundisha msimu ujao, baada ya kuibuka kwa taarifa za kuhitajika na Manchester United.

Enrique, ambaye kwa sasa ni mmoja kati ya makocha wakubwa barani Ulaya, akiwa ameshinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na Barcelona mwaka 2015 na Paris Saint-Germain mwaka 2025, amekuwa katika rada za Man United kwa muda sasa.

Kocha huyo Mhispania ametajwa kama mrithi anayeweza kuchukua mikoba ya Michael Carrick, ambaye kwa sasa ana mkataba na Man United hadi mwisho wa msimu huu.

Akiwa na PSG msimu huu, Enrique amekuwa na panda shuka nyingi, na sasa licha ya kuongoza ligi, ina tofauti ya pointi moja tu dhidi ya Lens iliyo nafasi ya pili.

Kwa mujibu wa tovuti ya The i Paper, vyanzo vya ndani ya PSG vinaamini kuwa Enrique atasaini mkataba mpya na klabu hiyo, wakati mkataba wake wa sasa ukitarajiwa kumalizika mwaka 2027.

Ripoti hiyo pia inaeleza kuwa Enrique yupo juu kwenye orodha ya makocha wanaoweza kuifundisha Man United, lakini kwa sasa Carrick bado ndiye anayepewa nafasi kubwa zaidi.

Mtendaji mkuu wa Man United, Omar Berrada na mkurugenzi wa michezo, Jason Wilcox, ndio wanaompendekeza sana Enrique, lakini wamiliki wao wanamwona Carrick kuwa chaguo linalofaa zaidi.

Wakati huohuo, inadaiwa kuwa Enrique anaweza akajiunga na Man City ikiwa timu hiyo itaachana na Pep Guardiola ifikapo mwisho wa msimu huu.

Katika mahojiano yake mwaka 2023, Enrique aliweka wazi kwamba siku moja angependa kufundisha klabu moja wapo katika ligi hiyo.

“Nafuatilia sana Ligi Kuu England kwa sababu ningependa kwenda kufanya kazi England. Sitaenda tu kwenye timu yoyote, bali ile inayoweza kufanya mambo makubwa.”