Lomancheko apewa dhahabu chungu balaa

BONDIA Vasyl Lomachenko hatimaye amekutana na bahati ya mtende ambayo akiipoteza atajilaumu mwenyewe kwani dalili kubwa zinaonyesha hatakuwa na nafasi nyingine ya kufanikisha lengo la kuwa bingwa wa mikanda minne (undisputed).
Lomachenko, bondia wa uzito wa light kutoka nchini Ukraine aliwahi kupata fursa ya kushinda mikanda minne ya uzito huo miaka kadhaa nyuma, lakini alishindwa kupigana na bondia George Kambosos Jr aliyekuwa anashikilia mikanda hiyo.
Hatimaye sasa fursa hiyo ameipata kutokana na kuwepo kwa pambano kati yake dhidi ya bondia Mmarekani Devin Haney ambaye ndiye anashikilia mikanda minne ya lightweight akiwa ni bondia hatari zaidi hata ya Kambosos. Pambano lao linatarajiwa kufanyika mwezi Mei.
Wakati Lomachenko akiwa na rekodi ya kushinda mapambano 17 yakiwamo 11 kwa ‘KO’ na kupoteza mawili, mpinzani wake Haney (undisputed) ana rekodi kali zaidi ya kushinda mapambano yote 29 aliyopigana yakiwemo 15 aliyoshinda kwa KO.
Mambo ni moto.