Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Liverpool yateseka, Arne Slot akiri ugumu

Muktasari:

  • Hadi kufikia wikiendi iliyopita Liverpool ilishapoteza mechi 10 msimu huu na ya mwisho ikiwa ni dhidi ya Brighton Jumapili ambayo ilimalizika kwa kichapo cha mabao 2-1.

LIVERPOOL, ENGLAND: KOCHA wa Liverpool, Arne Slot amesema yanayoendelea katika timu yake kwa msimu huu yanamuumiza sana kwani ni tofauti kabisa na matarajio yao.

Hadi kufikia wikiendi iliyopita Liverpool ilishapoteza mechi 10 msimu huu na ya mwisho ikiwa ni dhidi ya Brighton Jumapili ambayo ilimalizika kwa kichapo cha mabao 2-1.

Baada ya mechi Slot alionekana kuwa na huzuni sana na alipoulizwa kuhusu mwenendo wa timu yake alisema: “Kwa kweli inaumiza sana ukiangalia msimamo wa ligi. Tatizo kubwa ni kwamba tulipoteza pointi dhidi ya Wolves kwa bao lililogonga mchezaji na kubadilisha mwelekeo kisha wiki iliyopita tulilazimika kucheza mechi ngumu Jumapili dhidi ya Tottenham. Unajua tulikuwa mabingwa msimu uliopita kisha katika dirisha lililopita tukatumia Pauni 450 milioni hiyo ilisababisha matarajio kuwa makubwa kuanzia kwa wachambuzi, vyombo vya habari, mimi mwenyewe na mashabiki.”

“Bila kujali visingizio nitakavyotoa ukweli ni kwamba nafasi tuliyopo sasa si nzuri.”

Alipoulizwa kuhusu rekodi mbaya ya kupoteza mechi nyingi zaidi msimu huu kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2016 Slot alisema: “Inaonyesha mambo kadhaa. Kwanza inaonyesha jinsi Liverpool ilivyokuwa timu bora sana katika miaka 10 iliyopita pamoja na kocha mkubwa lakini kiuhalisia kuna sababu nyingi zinazoonyesha kwa nini tumepoteza mechi nyingi msimu huu. Tumekuwa tukiruhusu sana mabao katika dakika za mwisho hali inayoonyesha ufinyu wa kikosi chetu kutokana na idadi kubwa ya wachezaji majeruhi msimu huu. Kukosa wafungaji watatu muhimu ni janga kwenye timu yoyote ile bila kusahau kuumia kwa mabeki wetu wa kulia.”

“Lakini si kazi yangu kutafuta visingizio kazi yangu ni kutafuta suluhisho la matatizo kama hayo.”

Kipa Alisson naye kwa sasa yupo nje kutokana na majeraha ya misuli ya paja ambayo imesababisha pia asiitwe katika kikosi cha timu ya taifa ya Brazil.

Mshambuliaji Hugo Ekitike alipata jeraha la mguu katika mechi ya Brighton lakini halionekani kuwa kubwa na anaweza kuonekana katika kambi ya timu ya taifa ya Ufaransa wiki hii.

“Hugo angeweza kucheza kesho kama kungekuwa na mechi alipata maumivu tu kidogo yaliyotokana na mgongano uliomfanya atoke nje.”