Liverpool tano za Slot akikamiliza usajili wake

Muktasari:
- Jeremie Frimpong tayari ameshajiunga na miamba hiyo ya Anfield na kiungo Florian Wirtz anajiandaa kutua kwenye kikosi hicho kwa ada inayodaiwa kuwa itavunja rekodi ya uhamisho ya Uingereza ya Pauni 126 milioni.
LIVERPOOL, ENGLAND: LIVERPOOL huenda ikawa na sura mpya kabisa kwenye safu ya ushambuliaji baada ya kudaiwa kuwa na mkwanja wa Pauni 300 milioni wa kufanya usajili kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi.
Jeremie Frimpong tayari ameshajiunga na miamba hiyo ya Anfield na kiungo Florian Wirtz anajiandaa kutua kwenye kikosi hicho kwa ada inayodaiwa kuwa itavunja rekodi ya uhamisho ya Uingereza ya Pauni 126 milioni.
Lakini, mipango ya Liverpool chini ya kocha Mdachi, Arne Slot haipo kwenye kuishia wachezaji hao tu wawili.
Kinachoelezwa ni kwamba timu hiyo imepanga kufanya usajili wa kibabe wa ama kumnasa Alexander Isak wa Newcastle United au Bradley Barcola wa Paris Saint-Germain.
Isak bado yupo kwenye mipango ya Liverpool, lakini mabosi wa Newcastle hawapo tayari kumuuza staa huyo anayetajwa kuwa na thamani ya Pauni 150 milioni baada ya kukamatia tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Ikishindikana kumnasa Isak, basi itahamia kwa Barcola, anayedaiwa kuwa na thamani ya Pauni 100 milioni.
Sambamba na beki wa kushoto Milos Kerkez, anayetarajiwa kunaswa kwa Pauni 40 milioni, utafanya kikosi hicho cha Slot kuzidi kiwango cha Pauni 300 milioni. Kuweka vitabu kukaa sawa, washambuliaji Luis Diaz na Darwin Nunez wanaweza kuuzwa huku Barcelona na timu za Saudi Arabia zinahitaji huduma zao.
Kutokana na hilo, Liverpool inaweza kuwa na namna tano tofauti za kucheza kwenye Ligi Kuu England msimu ujao...
1. Chaguo la Kwanza; Kwenye kikosi hiki, Slot anaweza kuanza na mabeki wake wawili wapya wa pembeni. Frimpong na Kerkez watasaidia mashambulizi kuwasaidia Barcola na Mo Salah kwenye safu ya ushambuliaji. Kama Isak atashindwa kunaswa, basi Cody Gakpo ataongoza fowadi yake, wakati Wirtz atacheza nyuma yake.
2.Chaguo la Pili; Kama Liverpool itahitaji kufanya usajili mmoja tu kwenye dirisha hili kwenye eneo la fowadi, basi inaweza kumnasa Isak. Hiyo ina maana, Barcola hatasajiliwa na Wirtz au Luis Diaz atakuwa kwenye wingi ya kushoto. Kwenye chaguo hili, Slot ataendelea kutumia viungo wake watatu.
3.Chaguo la Tatu; Kuwasili kwa Frimpong kumempa Slot machaguo ya kutosha kwenye upande wa kulia. Staa huyo amekuwa akitumika kama wing-back wa kulia huko Bayer Leverkusen, akifunga mabao 30 na asisti 44 katika mechi 190. Beki huyo anapopanda mbele kushambulia anageuka na kuwa mshambuliaji hatari.
4.Chaguo la Nne; Kutakuwa na nafasi kubwa ya wachezaji wa kawaida kupata nafasi ya kucheza katika kikosi cha Liverpool msimu ujao. Kutokana na Caoimhin Kelleher kwenda Brentford, hiyo ina maana Giorgi Mamardashvili atakwenda kuwa chaguo la pili Liverpool.
5.Chaguo la Tano; Jarell Quansah ana matumaini makubwa ya kucheza kwenye chaguo hili la kocha Slot. Kukosekana kwa Isak hiyo ina maana Diogo Jota ataendelea kucheza kwenye safu ya ushambuliaji kwa sababu kwa kipindi hicho Barcola atakuwa nyongeza pekee kwenye safu hiyo ya washambuliaji watatu wa kikosi cha kocha Slot.
Timu zinazotajwa kumhitaji ni Aston Villa (timu yake ya zamani), Newcastle, Everton, West Ham na Napoli.