Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Abuya, Mudathir vitani na Aucho

VITANI Pict

APEWE nani? Hivyo ndivyo unaweza kusema. Hii ni baada ya eneo la kiungo mkabaji katika kikosi cha Yanga kutokuwa na uhakika wa kucheza msimu ujao, baada ya nyota wote wanaocheza nafasi hiyo kumaliza mikataba mwisho wa msimu huu.

Ipo hivi. Eneo la kiungo mkabaji la Yanga linaloongozwa na Khalid Aucho, Mudathir Yahya na Duke Abuya nyota hao wote mikataba yao inatamatika mwisho wa msimu ni mtihani kwa Yanga ni kupambana kuhakikisha inawabakiza wote au wawili kati yao kutokana na umuhimu ama rekodi tamu kikosini humo.

Yanga ilianza na Aucho kabla ya kumwongeza Mudathir na baadae Abuya na wote wameonyesha ubora wao katika kikosi hicho kila mmoja akipata nafasi ya kucheza huku mhimili mkubwa ukiwa ni mkongwe Aucho ambaye ameitumikia Yanga kwa misimu minne.

Aucho anayeitumikia Yanga kwa msimu wa tatu sasa, amekuwa mhimili wa timu hiyo chini ya makocha wanne tofauti kuanzia Naserddine Nabi, Miguel Gamondi, Sead Ramovic na sasa Miloud Hamdi na kwa sasa yupo nje ya uwanja kutokana na kuumia nyama za paja wakati wa mechi dhidi ya Coastal Union.

Wakati nyota huyo akijijengea ufalme dimba la chini Yanga, uongozi wa timu hiyo uliwaongeza Mudathir ambaye alianza kujiunga na Yanga na baadae Duke ambaye ameongeza ushindani eneo hilo hasa kwa Mzanzibar huyo ambaye msimu huu kasi yake imepungua tofauti na msimu wake wa kwanza.


VITA YA ABUYA, MUDA

Ujio wa Abuya Yanga umepunguza kasi ya Mudathir ambaye msimu huu ameshusha namba kwenye ufungaji, pia dakika za uchezaji kutokana na kupeana muda na nyota huyo.

Msimu huu Mudathir amecheza mechi 25 kati ya 27 za Yanga na hadi sasa ikisaliwa na michezo mitatu, huku mmoja ukiwa na sintofahamu kama utachezwa, kwenye mechi hizo amefunga mabao mawili, akitengeneza matatu na ametumika kwa dakika 1670.

Wakati kwa Abuya ametumika kwa dakika 1364 akicheza mechi 24 amefunga mabao mawili na kutengeneza mawili.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mudathir alisema anajivunia kuwa sehemu ya wachezaji wa Yanga waliotumika kwa kiasi kikubwa licha ya kutokuwa bora zaidi ya misimu miwili nyuma huku akiweka wazi ushindani wa namba umechangia.

“Uwepo wa Abuya na ubora wa safu ya ushambuliaji msimu huu umechangia namba zangu kupungua, lakini najivunia hilo kwani nimehimili ushindani kwa kupata nafasi ya kucheza licha ya kuongezwa kwa wachezaji eneo ninalocheza nafurahia ushindani unaniongezea ubora,” alisema na kuongeza;

“Ukiongezewa namba ya wachezaji eneo unalocheza unakua kiuchezaji, nimepenya kikosi cha kwanza mbele ya makocha wanne tofauti waliopita Yanga nikianza na Nasreddine Nabi, kwangu ni ushindi pia nafurahia ushindani nilioupata umeniongezea kitu kwenye kuboresha kiwango changu;

“Ubora wa mchezaji mmoja mmoja ndani ya kikosi cha Yanga umekua chachu kubwa ya mimi kujiweka kwenye ushindani kwa sababu nikiamini kuwa nipo fiti na nina uhakika wa namba, hivyo juhudi na maarifa naviongeza kwenye kila mchezo pale ninapopata nafasi ya kucheza naheshimu ubora wa wachezaji wote wanaocheza eneo ninalocheza.”

Nyota wengine wanaocheza eneo hilo na hawana uhakika wa namba kikosi cha kwanza ni Jonas Mkude ambaye pia mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu huu, Aziz Andabwile ambaye yupo kwa mkopo na Salum Abubakar ‘Sure Boy’.