Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Liverpool, Newcastle United watauana

WATAUANA Pict

Muktasari:

  • Majogoo hao wako tayari kuvuruga mpango wa Magpies wa kumsajili mshambuliaji huyo wa Kifaransa mwenye umri wa miaka 23, baada ya kuambiwa kuwa chaguo lao la kwanza Alexander Isak hauzwi kwa bei yoyote na klabu hiyo.

LIVERPOOL, ENGLAND: LIVERPOOL imetangaza vita dhidi ya Newcastle kwa kutaka kumnyakua Hugo Ekitike kutoka Eintracht Frankfurt katika dirisha hili.

Majogoo hao wako tayari kuvuruga mpango wa Magpies wa kumsajili mshambuliaji huyo wa Kifaransa mwenye umri wa miaka 23, baada ya kuambiwa kuwa chaguo lao la kwanza Alexander Isak hauzwi kwa bei yoyote na klabu hiyo.

Liverpool ilikuwa tayari kutoa dau kubwa la rekodi ya Uingereza la Pauni 120 milioni kwa ajili ya kumpata Isak mwenye umri wa miaka 25 lakini bado Newcastle wanadaiwa kukataa.

Lakini sasa kocha Arne Slot yupo tayari kuchukua hatua ya kishujaa na kupiga bomu kwenye mipango ya Newcastle ambayo inataka kumsajili Ekitike ili acheze sambamba na Isak.

SunSport imefichua kuwa Liverpool imewasiliana rasmi na klabu hiyo ya Ujerumani kuanza mazungumzo ili kujiandaa kumnunua Ekitike.

Isak ambaye mkataba wake unamalizika mwaka 2028, licha ya kutamani kuondoka lakini ripoti zinadai hatolazimisha kufanya hivyo.

Liverpool ilivutiwa sana na kiwango cha Isak ambaye msimu uliopita aling'ara na kuisaidia timu hiyo kushinda taji lao kubwa la kwanza baada ya miaka 70 na pia kuiwezesha kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Mbali ya kukataa kumuuza, Newcastle pia imepanga kufanya haraka kumsainisha mkataba mpya ambao utamwezesha kupata zaidi ya Pauni 150,000  kwa wiki kutoka mshahara wa Pauni 130,000 anaoupata kwa sasa.

Inaelezwa kocha Eddie Howe ndio hataki staa huyu auzwe na ndoto yake ilikuwa ni kuanzisha safu tamu ya ushambuliaji ambayo itaundwa na Anthony Elanga, Isak pamoja na Ekitike ikiwa atasajiliwa.

Howe amekuwa akihitaji huduma ya Ekitike tangu mwaka 2022 ambapo alichagua kujiunga na PSG badala ya Newcastle.

Frankfurt ilikataa ofa ya Pauni 70 milioni kutoka Newcastle kwa ajili ya Ekitike Jumanne ya wiki hii na kusisitiza kwamba wanahitaji Pauni 86 milioni.