Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Liverpool itachangamka! Arne Slot kufunga busta

SLOT Pict
SLOT Pict

Muktasari:

  • Liverpool bado haijanyakua taji la Ligi Kuu England msimu huu, lakini imejiweka kwenye mazingira mazuri ya kulibeba na kinachosubiriwa ni kuthibitishwa tu kuwa ni mabingwa wapya.

LIVERPOOL, ENGLAND: LIVERPOOL imepanga kufungulia pochi dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi ili kumpatia Kocha Arne Slot kikosi kitakachokuwa na uwezo wa kutetea taji la Ligi Kuu England watakalolibeba msimu huu.

Liverpool bado haijanyakua taji la Ligi Kuu England msimu huu, lakini imejiweka kwenye mazingira mazuri ya kulibeba na kinachosubiriwa ni kuthibitishwa tu kuwa ni mabingwa wapya.

Hilo lilikamilika, mipango yote itahamia msimu ujao na tayari imeshafahamu usajili itakaofanya ili kufanya kikosi hicho kuwa cha kibeba kabisa na kuwa na nguvu ya kutetea taji.

Kwenye kikosi hicho cha Liverpool kuna mastaa kama Mohamed Salah, Virgil Van Dijk na Trent Alexander-Arnold mikataba yao itafika ukomo mwisho wa msimu, lakini mabosi wa miamba hiyo ya Anfield bado hawajakata tamaa, wanaamini watafanikiwa kuwasainisha dili mpya kabla ya mkataba huu kufika tamati.

Lakini, kama itashindwa kufanya hivyo, basi italazimika kuingia sokoni kufanya usajili wa maana. Tayari kuna majina kadhaa ya wachezaji wanaowindwa na miamba hiyo ya Anfield kabla ya dirisha la usajili halijafunguliwa.

Kwenye safu ya ulinzi, kutakuwa na mabadiliko machache kwenye kikosi. Kwanza kwenye beki ya kulia, Alexander-Arnold anapiga hesabu za kwenda Real Madrid. Kwenye hilo, Liverpool inamtaka beki wa Bayer Leverkusen, Jeremie Frimpong kuja kuziba pengo lake endapo kama atakwenda Bernabeu.

Liverpool pia inaweza kumnasa Pedro Hincapie, ambaye atakuja kumrithi Ibrahima Konate kwenye nafasi ya beki ya kati, wakati huo kwa upande wa kushoto, beki wa Bournemouth, Milos Kerkez, anaweza kunaswa na miamba hiyo ya Anfield. Beki wa kati, Virgil van Dijk, naye mkataba wake unaisha, lakini matumaini makubwa atabaki.

Kwenye sehemu ya kiungo, Liverpool haitakuwa na mabadiliko makubwa na Dominik Szoboszlai na Alexis Mac Allister sambamba na Ryan Gravenberch wataendelea kuwa sehemu muhimu ya safu hiyo ya kiungo.

Liverpool imeripotiwa kuwa na mpango pia wa kumsaka mshambuliaji wa Bournemouth, Antoine Semenyo. Katika kuifanya fowadi yao kuwa matata zaidi, kinachoelezwa Liverpool inamtaka pia straika wa Bayern Munich, Harry Kane.

Kama itafanikiwa kumnasa Kane na kisha Mo Salah akasaini dili la kubaki, safu ya ushambuliaji ya Liverpool itakuwa ina balaa kubwa huko Anfield msimu ujao.

Liverpool XI: Alisson; Kerkez, Van Dijk, Hincapie, Frimpong; Gravenberch, Mac Allister, Szoboszlai; Salah, Semenyo, Kane.