Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mastaa wapya hatihati Chelsea

MASTAA Pict

Muktasari:

  • Matajiri hawa wa Jiji la London, tayari wametumia zaidi ya pauni 160 milioni kwa ajili ya kuwasajili Delap, Pedro, kijana wa Kibrazili Willian Estevao, Jamie Gittens  na wachezaji wengine katika dirisha hili.

LONDON, ENGLAND: CHELSEA inaweza kupigwa marufuku kuwatumia Liam Delap, Joao Pedro na wachezaji wengine iliowasajili majira haya ya kiangazi katika Ligi ya Mabingwa msimu ujao.

Matajiri hawa wa Jiji la London, tayari wametumia zaidi ya pauni 160 milioni kwa ajili ya kuwasajili Delap, Pedro, kijana wa Kibrazili Willian Estevao, Jamie Gittens  na wachezaji wengine katika dirisha hili.

Hata hivyo, ikiwa  haitofanikiwa kusawazisha hesabu zao kwa kuuza au kuwatoa kwa mkopo wachezaji kabla ya dirisha kufungwa, masharti ya adhabu yao ya UEFA kwa kuvunja kanuni za kifedha yatazuia wachezaji hao kusajiliwa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa msimu ujao.

Wiki iliyopita shrikisho la soka barani Ulaya ‘UEFA’  iliitoza Chelsea faini ya jumla ya pauni 27 milioni kwa kukiuka kanuni hizo.

Baada ya kupigwa faini hiyo, kama sehemu ya maelekezo Chelsea iliambiwa kuwa haitowezi kuongeza wachezaji kwenye orodha ya wachezaji 25 watakaocheza UEFA msimu ujao bila kufidia gharama za kila mchezaji mpya kwa kuondoa mchezaji mwingine wa thamani sawa katika orodha ya zamani.

Gharama ya kila mchezaji kwa mwaka huhesabiwa kwa kujumlisha mshahara wake na thamani ya usajili wake inayogawanywa kwa miaka mitano.

Kwa mfano, Delap ambaye amejiunga akitokea Ipswich kwa ada ya pauni 30 milioni kwenye mkataba wa miaka sita, thamani yake inapigiwa mahesabu kwa miaka mitano, hivyo pauni 30 milioni ikigawanywa na kupatikana pauni 6 milioni, huunganishwa pia na mshahra ambao anauapata kwa mwaka, hivyo kwa pauni 100,000 kwa wiki jumla anakunja pauni 5.2 milioni kwa mwaka.

Katika mjumuisho, thamani ya staa huyu jumla ni pauni 11.2 milioni.

Hivyo, Iwapo Chelsea inataka Delap acheze Ligi ya Mabingwa, itabidi iondoe mchezaji ambaye thamani yake iwe sawa na thamani ya Delap au izidi.

Thamani ya mchezaji anayeondoka huhesabiwa kwa kujumlisha mshahara wake na faida yoyote inayotokana na uuzwaji wake.

Ikiwa Chelse itaondoa mchezaji ambaye ilimnunua  kama kipa Robert Sanchez, hesabu zinabadilika.

Sanchez alisajiliwa kutoka Brighton kwa pauni 25 milioni miaka miwili iliyopita. Gharama ya usajili kwa kila mwaka ni pauni milioni 5, hivyo kwa miaka miwili aliyohudumu hadi sasa thamani yake imefikia pauni 10 milioni na pamoja na mshahara imefikia pauni 15 milioni, hivyo Chelsea inahitaji kumuuza kwa zaidi ya kiasi hicho ili kupata nafasi ya kuingiza wengine kwa sababu kitakachozidi ndio kitahesabika kama faida.

Hata hiyo, ikimuuza mchezaji kama Trevoh Chalobah itakuwa faida sana kwao kwani  ni zao la akademi ya Chelsea, thamani yake ya kibenki ni sifuri, hivyo ada yoyote ya uhamisho itakayopatikana itahesabiwa kama faida.

Hali kama hiyo ilitokea ilipomuuza Mason Mount na Conor Gallagher  miaka miwili iliyopita.

Ikiwa itafanikiwa kumuuza kwa Chalobah kwa ada ya pauni 40 milioni pamoja na mshahara wake, Chelsea inaweza kufidia gharama za Delap na Joao Pedro ambao wataweza kuingia katika kikosi cha Ligi ya Mabingwa lakini bado kutakuwa na kundi lengine la wachezaji.