Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ligi Kuu za Ulaya ni mchakamchaka

Muktasari:

  • Kwenye Ligi Kuu England, Manchester United itakuwa ugenini kukipiga na Brentford, wakati Brighton itakipiga na Newcastle United, West Ham United na Tottenham Hotspur na kazi nyingine itakuwa huko Stamford Bridge, wakati Chelsea itakapokutana na mabingwa, Liverpool.

LONDON, ENGLAND: MCHAKAMCHAKA wa Ligi Kuu za Ulaya unaendelea kupamba moto, kuanzia kwenye Ligi Kuu England, La Liga, Bundesliga, Serie A na Ligue 1. Ni balaa.

Kwenye Ligi Kuu England, Manchester United itakuwa ugenini kukipiga na Brentford, wakati Brighton itakipiga na Newcastle United, West Ham United na Tottenham Hotspur na kazi nyingine itakuwa huko Stamford Bridge, wakati Chelsea itakapokutana na mabingwa, Liverpool.

Mechi hizo zote zitafanyika Jumapili, kama ilivyo kwenye ligi nyingine, ambako huko La Liga, Real Madrid itakuwa nyumbani kucheza na Celta Vigo, huku Sevilla ikiwa na kazi mbele ya Leganes, Espanyol na Real Betis na Real Sociedad itakipiga na Athletic Bilbao.

Kwenye Bundesliga, Augsburg itakuwa nyumbani kucheza na Holstein Kiel, wakati Xabi Alonso na chama lake la Bayer Leverkusen atakuwa ugenini kukipiga na Freiburg, huku Mainz 05 itakuwa na kibarua kizito mbele ya Eintracht Frankfurt.

Huko Serie A nako hapatoshi, mchakamchaka utazikutanisha Empoli na Lazio, huku Monza ikikipiga na Atalanta na AS Roma itakuwa na kasheshe zito mbele ya Fiorentina na Bologna itakuwa mwenyeji wa kukabiliana na vigogo wa ligi hiyo, Juventus.

Kwenye Ligue 1, kutakuwa na mechi tano Jumapili, ambapo Nantes itakuwa nyumbani kucheza na Angers, wakati Auxerre itamaliza ubishi na Le Harve, huku Brest ikiwa na kazi mbele ya Montpellier, Lyon ikicheza na Lens na Lille itakuwa na shughuli pevu kwa kukabiliana na Marseille katika moja ya mechi zinazotazamiwa kuwa na upinzani mkali kwenye ligi hiyo.