Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

'Mbongo' aitibulia Bayern pati la ubingwa 

YUSUF Pict

Muktasari:

  • Bayern ilikuwa inahitaji ushindi ili kutangazwa bingwa wa Bundesliga na mambo yalionekana kuwanyookea walipopindua meza kutoka ya mabao 2-0 kuonekana kama wangeibuka na ushindi wa 3-2 kabla Poulsen ambaye mmoja wa wazazi wake ni Mtanzania kutoka Tanga kuchomoa bao hilo na kuifanya iahirishe pati la ubingwa.

PATI la ubingwa la klabu ya Bayern Munich, imetibuliwa Ujerumani baada nyota mwenye asili ya Tanzania, Yussuf Poulsen kufunga la la kusawazisha sekunde chache kabla ya filimbi ya mwisho na kuiwezesha RB Leipzig kitoka sare ya 3-3 ikiwa nyumbani jioni hii.

Bayern ilikuwa inahitaji ushindi ili kutangazwa bingwa wa Bundesliga na mambo yalionekana kuwanyookea walipopindua meza kutoka ya mabao 2-0 kuonekana kama wangeibuka na ushindi wa 3-2 kabla Poulsen ambaye mmoja wa wazazi wake ni Mtanzania kutoka Tanga kuchomoa bao hilo na kuifanya iahirishe pati la ubingwa.

Bayern ikiwa na pointi tisa zaidi mbele ya Bayer Leverkusen inayoshikilia ubingwa kwa sasa ikiwa imebakiza  mechi tatu.
Leipzig iliongoza kwa 2-0 kwa mabao ya Benjamin Sesko na Lukas Klostermann, kabla ya Bayern kurudi mchezoni kipindi cha pili kupitia Eric Dier na Michael Olise, na baadaye Leroy Sane kufunga la tatu.
Hata hivyo, Yussuf Poulsen alisawazisha sekunde za mwisho na kuzuia Bayern kushinda taji siku hiyo. Bayern sasa inahitaji pointi mbili katika mechi mbili ilizonazo mkononi kufungia msimu ili kurejesha taji hilo.

Hata hivyo, kazi inaweza kuwa rahisi kama tu, Leverkusen itapoteza leo ugenini dhidi ya Freiburg  na kuifanya Bavarian  watwae taji lao la 12 katika misimu 13.

Bila ya kuwepo kwa Harry Kane, uwanjani  vijana wa Vincent Kompany walikuwa na imani ya kutangaza ubingwa ugenini ili kumfariji straika na nahodha huyo wa England ambaye hajawahi kutwaa taji lolote kubwa katika maisha yake ya soka, lakini mabao mawili ya kipindi cha kwanza kuwatungisha.

Wenyeji RB Leipzig  waliwazidi kwa nafasi za mapema.
Dakika ya 11 Xavi Simons alimnyang'anya mpira Michael Olise na kwa ustadi mkubwa akatumia nje ya kisigino chake kumpasia Benjamin Sesko, ambaye alimzidi maarifa Urbig aliyekuwa mbali na lango na kufunga bao zuei kwa shuti la mbali.

Bayern ilirudi mchezoni kwa kumiliki  lakini dakika ya 39  ikajikuta ikifungwa bao la pili kupitia kwa David Raum alipiga mpira wa adhabu kutoka mbali, na Lukas Klostermann alimtoroka beki wake na kutumbukiza wavuni.

Katika kipindi cha pili, Bayern ilirudi kivingine na kufanya mashambulizi makali na kusawazisha mabao yote mawili kwa kutumia dakika moja tu, dakika ya 62 iliandika bao la kwanza baada ya
Eric Dier kurukia mpira wa kona iliyopigwa na Olise, na kupiga mpira uliotinga upande wa karibu wa goli, kabla ya Olise kufunga bao la pili sekunde 46 tu baadaye. 

Leipzig ilipoteza mpira mara moja baada ya kuanza, na Serge Gnabry akampasia Olise aliyepiga shuli kali kali.

Bao la tatu lilionekana kuwa la ushindi kwa Bayern, lilitokana na Joshua Kimmich alipouelekeza mpira kwa Leroy Sane, aliyepokea na kupiga kwa ustadi hadi kona ya mbali ya goli dakika ya 83.

Dakika ya 90+5, wakati mashabiki wa Bayern wakiendelea kushangweka kaa kuamini kazi imeisha ndipo 'Mdigo' Yussuf Poulsen alipokea paai tamu kutoka kwa Xavi na kumpiga chenga Urbig na kutumbukiza mpira wavuni ma kufanya matokeo kuwa mabao 3-3.

Bayern imeifika pointi 76 kupitia mechi 32, wakati Leverkusen inashika nafazi ya pili ikiwa na pointi 67 kwa mechi 31 na RB Leipzig kwa matokeo hayo ya leo, imefikisha pointi 50 kupitia mechi 32 ikisalia nafasi ya tano, nyuma ya Freiburg itakoikaribisha Leverkusen leo jioni.